OBAMA AOMBA MSAADA WA $3.7 BILIONI
Rais Obama anaomba dola bilioni 3.7 za msaada wa
dharura kutoka bunge la Marekani kusaidia kukabiliana na ongezeko la
watoto waliohama peke yao kutoka Amerika ya kati.

Ikulu ya Marekani inasema fedha hizo zitasaidia
kupunguza kile maafisa wanakitaja kuwa hali ya dharura ya kibinaadamu
iliyoshuhudia watoto zaidi ya elfu hamsini na mbili waliohama peke yao
kutoka El Salvador, Guatemala na Honduras kuvuka kiharamu mpaka wa
Marekani tangu mwezi Oktoba mwaka jana.
Umaskini na ongezeko la hivi
karibuni la ghasia zinazohusiana na magenge na mitandao ya ulanguzi
madawa ya kulevya zimesababisha ongezeko la wahamiaji kutoka eneo hilo
la Amerika ya kati.
Wengi wao watoto ambao wameingia Marekani kupitia bonde la Rio Grande huko Texas.
Wengi wao watoto ambao wameingia Marekani kupitia bonde la Rio Grande huko Texas.
Wengi wanazuiwa katika vizuizi vilivyo jaa watu wakati maafisa wanang'ang'ana kukabiliana nao.
Rais Obama ameielezea hali kuwa mzozo wa
kibinaadamu na sasa anaomba mabilioni ya dola kutoka bunge nchini humo
kuharakisha kushughulikiwa na kusafirishwa kwa wahamiaji hao, vile vile
kuongeza ukaguzi na kuyasaka makundi ya kihalifu yanayosaidia
kusafirishwa kiharamu kwa wahamiaji katika mpaka.
Kampeni katika vyombo vya habari katika nchi
wanazotoka wahamiaji hao, inatarajiwa pia kuondosha fikra kwamba watoto
wanaowasili Marekani kiharamu wataruhusiwa kukaa.
Licha ya makubaliano kwamba mfumo huo unahitaji
mageuzi ya dharura, bunge limetatizwa na iwapo wabadilishe mfumo mzima
wa uhamiaji nchini.
OBAMA AOMBA MSAADA WA $3.7 BILIONI
Reviewed by Unknown
on
01:19:00
Rating:
