HATARI: HIVI NDIVYO DADA ZETU WA KITANZANIA WANAVYOTUMIKISHWA KATIKA KUUZA MIILI YAO HUKO CHINA
hali sasa ni tofauti kwa kuwa kuna wasichana ambao huenda huko kwa ahadi za ajira, lakini huishia kufanya ukahaba kwenye madanguro, gazeti hili linaweza kukuthibitishia.
Wasichana hao hutafutwa na mawakala wa hapa nchini ambao
kazi yao huwa ni kutafuta wasichana wazuri na baadaye kuwashawishi kwa
kuwaeleza fursa za ajira za hotelini zilizo barani Asia.
Msichana akikubali, wakala huchukua jukumu la kumtafutia
viza ya kuingia China na baadaye kuwasiliana na mwenyeji wake, maarufu kama
Lady Boss, ambaye hutuma tiketi ya ndege kwa ajili ya kumsafirisha ‘mwajiriwa’
mpya.
Alisema alipotoka Dar es Salaam aliambiwa angepokewa na mtu
anayeitwa Jacky ambaye hakumkuta kwa kuwa alikuwa safarini Malaysia, lakini
alikuwa ameacha maagizo apokewe na mwanamke mwingine.
“Nilielekezwa nikodi
taksi hadi kwenye hoteli inayoitwa Nairobian. Kutoka hapo uwanja wa ndege
hadi kwenye hiyo hoteli ni sawa na
umbali wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hadi Bagamoyo,”
anasema Munira.
Anasema alitakiwa
kulipa Yuan 200 (Sh60,000) na alipofika katika hoteli hiyo alipokewa, akaoga na
kupewa chakula.
“Nilipomaliza kula
nilipumzika kwa saa mbili hivi. Jacky alikuwa amesharudi na alinifuata chumbani
na kuniambia natakiwa kwenda saluni. Hivyo tuliondoka pamoja hadi kwenye jengo
kubwa lenye maduka makubwa linaloitwa Tin- shu,” anasimulia Munira.
Watanzania lukuki
Katika jengo hilo alishangaa kuwaona Watanzania wengi,
wakiwamo wanawake kadhaa ambao aliwahi kukutana nao Magomeni wakati akifuatilia
safari yake.
Munira anasema miongoni mwa watu aliowaona ni binti mmoja
ambaye wanafahamiana ambaye alistaajabu kumwona sehemu hiyo.
“Aliniuliza kwa
mshangao, ‘mbona umekuja huku? Umekuja kufanya nini?’ Wakaanza kunishangaa.
Yule msichana akaniambia ‘huku msala ndugu yangu, umekuja kufanya nini?”
alimnukuu na kuongeza kuwa kabla hawajamaliza mazungumzo yao, mwenyeji wake
alitokea hivyo waliyakatisha.
Anasema waliingia saluni ambako aliwakuta Watanzania na
Wakenya wakifanya kazi humo na wakati yeye akiendelea kusukwa nywele kwa
umaridadi, Jacky alikwenda kumnunulia nguo na viatu dukani.
“Baada ya hapo
niliambiwa nivae nguo niende klabu kwa sababu huo ni msimu wa sikukuu za mwaka
mpya wa Kichina,” alisema Munira.
Anasema alishangaa kuambiwa aende klabu usiku huo wakati
alikuwa amechoka kwa safari ndefu.
“Kilichokuwa kinanipa
moyo usiku ule ni kuwa niliwaona wasichana wa Magomeni, lakini nilihisi
wameambiwa wasiwe karibu na mimi.”
Hata hivyo, hali hubadilika mara wafikapo huko kwa kuwa
‘mwajiri’ huyo humpokonya hati ya kusafiria na baadaye kumpa maelekezo kuwa
atatakiwa kulipa Dola 200 kila siku ambazo atakuwa akizipata kwa kufanya
umalaya kwenye klabu na maeneo ya biashara.
Tayari wasichana kadhaa wa Kitanzania wamenaswa katika mtego
huo na kujikuta wakilazimika kuuza miili yao ili wamudu ada ya Dola 200 pamoja
na fedha za kujikimu, akiwemo Munira Mathias mwenye umri wa miaka 23 ambaye
alimudu kuvaa ujasiri wa kuweka bayana uovu huo katika mazungumzo yake na
gazeti hili.
Binti huyo Mtanzania aliyesafiri kwa saa 18 kwenda Guangzou,
China alitakiwa kupumzika kwa saa mbili tu kabla ya kupelekwa kuanza ‘kazi’
ambayo hakuitarajia.
“Baada ya kupumzika
kwa saa mbili tu, nilipelekwa kwenye klabu,” anasema Munira wakati akisimulia
mkasa wake.
“Sikuwa na kazi
nyingine zaidi ya kucheza muziki na wanaume ambao licha ya kwamba sikuwahi
kuwaona, walinichangamkia kama vile wananifahamu.”
Munira aliondoka Januari mwaka huu kwenda China ambako
aliahidiwa kuwa angeajiriwa hotelini, lakini alikutana na ‘ajira’ ya ukahaba,
huku akilazimika kuwalipa ‘waajiri’ wake Dola za Marekani 200 kila siku.
Binti huyo, ambaye
alifanikiwa kuchomoka mikononi mwa waajiri hao baada ya viza yake kuisha, alisema
kwa siku 91 alizokaa China, alipata mateso ambayo hatayasahau ikiwamo kupigwa,
kubakwa na kundi la wanaume raia wa Nigeria, pia kulazimika kutoa mimba
aliyoipata kwa kubakwa.
“Nilifika Guangzhou
kama saa 9.00 alasiri za China na kulikuwa na baridi sana,” anasema Munira
akisimulia jinsi alivyokanyaga kwa mara ya kwanza ardhi ya nchi hiyo akiwa na
matumaini ya kuanza maisha mapya.
“Wakati huo nilikuwa nikijaribu kupata mawasiliano na
mwenyeji wangu ambaye niliagizwa kutoka Magomeni, Dar es Salaam.
Anasema alipoingia klabu, pia alishangaa zaidi kukutana na
Watanzania wengi wa rika tofauti ambao baadhi yao aliwatambua kwa sura na pia
kulikuwa na raia wengi wa Nigeria.
“Kiasi fulani
nilifarijika kuwaona Watanzania na nilijisikia kukua kiakili baada ya kuwaona
Wanigeria ambao nilizoea kuwaona kwenye filamu peke yake,” anasema.
Hata hivyo, alishangaa kuona pale klabu alichangamkiwa na
watu wengi, lakini hakutaka kudadisi zaidi bali alidhani ndiyo hali halisi au
alikuwa na bahati ya kupendwa.
“Baada ya kumaliza
kucheza muziki kwenye klabu hiyo, walipelekwa kwenye klabu nyingine ya asubuhi.
“Tuliporudi hotelini, nilijitupa kitandani na kulala kwa
sababu ya uchovu mwingi. Miguu ilikuwa imevimba kwa sababu nilikuwa
nimevalishwa viatu virefu na kucheza muziki mfululizo. Nikalala bila ya hata
kuoga,” anasema.
Mwanzo wa mateso
Baada ya saa moja kupita na akiwa amelala fofofo mchana ule,
mara aliamshwa na Jacky, ambaye alimwamuru amkabidhi pasipoti yake.
“Nikampa, pasipoti
yangu nilikuwa nimeiambatanisha na tiketi na kila kitu. Akanishangaza kuniambia
kuwa kuanzia siku hiyo niwe nampelekea Dola 200 mezani kila siku. Nilishangaa
na nikaanza kulia,” anasema.
Kwa hasira na mshtuko
alioupata, Munira anasema alitoka nje na kuanza kulia na wenzake walipomuuliza
kinachomliza, aliwaeleza. Waliamua kumwambia ukweli kwamba hata wao walipelekwa
kwa miadi ya kupata ajira za hoteli, lakini hawafanyi hivyo.
“Waliniambia kuwa nao
walirubuniwa na wakanyang’anywa hati za kusafiria kama mimi na wakaishia
kuambiwa wafanye biashara ya kuuza miili ili watafute fedha,” anasema Munira.
Munira anasema
alichanganyikiwa, hasa pale alipoambiwa na wenzake kwamba kazi kubwa ni kwenda
klabu kujiuza au kuzurura eneo la Chambu Chambu.
Chambu Chambu ni soko
la bidhaa ambako wasichana hujifanya wananunua vitu, lakini kimsingi huwa
wanakwenda kutafuta wateja wa ngono.
Kule wanaume wameshajijengea picha kuwa wanawake wa
Kitanzania wapo kwa ajili ya kujiuza, basi wakikuona tu wanakufuata na mnaongea
biashara, mnakwenda kumalizana,” anasimulia.
Wasichana wenzake wa
Kitanzania walimwambia kuwa hayo ndiyo maisha yenyewe, hivyo aliporejea ndani,
mwenyeji wake (Jacky) alimwambia ajiandae kuanza kazi mara moja na Munira akawa
hana budi kufuata maelekezo.
Baada ya hapo aliingia bafuni akaoga, kisha akaenda eneo la
Chambu Chambu kutafuta wateja.
“Nikakubaliana na
hali halisi nikawa nafanya kazi kama nilivyoambiwa. Niliona nikubali lakini
akili kichwani mwangu ilikuwa nifanye mbinu ili nirudi nyumbani,” anasema.
Simulizi ya Munira itaendelea kesho kwenye kijarida cha
Ndani ya Habari.
Primary Source: Munira
Mathias si jina halisi-Mhariri
HATARI: HIVI NDIVYO DADA ZETU WA KITANZANIA WANAVYOTUMIKISHWA KATIKA KUUZA MIILI YAO HUKO CHINA
Reviewed by Unknown
on
01:15:00
Rating:
Reviewed by Unknown
on
01:15:00
Rating: