Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa


Natanguliza kutoa pole kwa familia,ndugu, jamaa na Marafiki wa familia ya kapt Komba bila kuwasahau wananchi wa Mbinga ambao marehemu alishawakimbia muda mrefu anaishi dar Kwenye kiyoyozi muda wote leo wanapata mshtuko mkubwa kuambiwa mbunge wao amewatoka hakika ni majonzi makubwa sana.

Hapa nawalenga wanasiasa wetu, ni vema kila mwanasiasa akajitathmini, msisahau siasa ni Karama tulizogawiwa na M/Mungu kama zilivyo karama zingine.

Ndugu zangu Mwenyzi Mungu ametupa utashi wa kupambanua mambo tofauti na wanyama.....
Lakini pia mkumbuke kila mtu hapa duniani atakumbukwa tu Mara baada ya kututoka but style za kukumbukwa huwa zinatofautiana, either utakumbukwa kwa mabaya yako ulipokuwa hai au kwa mazuri yako.

Ndugu wanasiasa wengi wenu mmekuwa mkijisahau sana kwamba pia kuna maisha out of politics but ukweli ni kwamba wew kufa hakukuondolei ukweli wa yale uliyokuw ukiyafanya kipindi cha uhai wako.

Hapa ninachokilenga ni kwamba kifo cha Kapt Komba kimeibua hisia tofauti ndani ya jamii, wengi wamekuwa wakiona ni sahihi huyu Mzee kupunzika, wengine wakisema kauli zake zilikuwa za kuudhi na kutaka kuchafua nchi..... Lakini kundi la pili likidai watu kumsema marehemu siyo sahihi inajenga image mbaya kwa jamii....

Ukweli ni kwamba kifo isitumike kama mwavuli wa kuficha mabaya ya mtu, hii ni dalili ya uwoga watu kuogopa kuhukumiwa baadae huko ahera kwa kusema mabaya ya marehemu... Ukweli hauwezi kubadilishwa kwani hakuna binadamu asiyejua kuwa kuna kifo na maandalizi ya maisha ya mtu ni yake mwenyewe tuache uwoga usiokuwa na maana, tutakukumbuka na kuyasema kwa yale uliyokuwa ukiyafanya enzi za uhai wako, mazuri yako tutayasifia na mabaya pia tutayasema na kuyalaani.

Ushauri wangu.

Wanasiasa wetu mmekuwa mkijisahau sana as if vifo haviwahusu nyie, please kila mmoja wenu ayatafakari maisha yake ya kisiasa na kujiuliza Je utakumbukwa kwa lipi??? Tumieni ndimi zenu vyema huku mkitambua kuwa kauli zenu zina impact kubwa sana kwa jamii.

KUMBUKENI KILA MMOJA HAPA DUNIANI ATAKUMBUKWA KWA STYLE YAKE.

THANKS
Ni hayo tu.
Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa Reviewed by CapchaMuzic on 01:03:00 Rating: 5
Powered by Blogger.