Jinsi ya kumwita jini na kumuamrisha unavyotaka. Awe rafiki, mpenzi au msaidizi


Naam, nimekuja tena kupamba jukwaa kwa aina ya pekee kabisa.

Nadhani mmewahi kusikia juu ya hawa viumbe wanaoitwa MAJINI. Mmesikia stori mbalimbali kuwahusu lakini leo sio stori tena na vitendo.

Hawa ni viumbe wanaoishi ktk ulimwengu wao wa majini. Kuna geti/lango kubwa sana linalotenganisha dunia yetu na wanayoishi wao.

Leo nitawafafanulieni namna ya KUTENGENEZA JINI na umtumie kama rafiki, mpenzi au msaidizi wako pasipo kukudhuru.

http://www.drsharma.ca/wp-content/uploads/sharma-obesity-witch-doctor.jpgMAHITAJI/VIFAA.

-Udi 4 (4 incense sticks).
-Pete, cheni. (ring or chain).
-Mishumaa 3. mweupe, mweusi na mwekundu.
-Muda ni saa 6-10 usiku mwezi ukiwa mpevu.
-Chumba tupu na kisafi.
-kioo.
-lipstick nyeusi/nyekundu.

HATUA ZA KUFUATA.

1. Ingia ktk chumba ulichoandaa ktk muda ulitajwa hapo juu ukiwa na vifaa vyote. Choma udi yote kisha toka nje hadi imalizike kuungua kisha rudi tena chumbani.

2. Kaa sakafuni kisha pangaa mishumaa yako mbele yako kwa kufuatana ukianza kushoto kwenda kulia. Anza na mshumaa mweupe, mwekundu kisha mweusi(nafasi kati ya mshumaa hadi mshumaa ni inchi 6(6 inches).

3. Sema maneno haya mara 6 "ALLAH SHAFIM BARAT SHIU KAMIR". Maneno hayo hutumika kufungta geti la kule ulimwengu wa majini. Hapo unakuwa umefungua geti tayari.

4. Washa mishumaa yako ukianza na mweupe, mweusi kisha mwekundu. (kila rangi ina maana yake, nyeupe inasimama badala ya amani, nyeusi ni ulimwengu wa kijini na nyekundu ni made material yao kwani wameumbwa kwa moto).

5. Chagua aina ya jini umtakaye na jinsia yake. Chukua kioo chako sasa kisha andika maneno haya katikati ya kioo kwa kutumia lipstick yako, "ALI ALLAH HAMAL JINNI". Kisha kisha andika jinsia yake MUSCHNA(Kwa jini wa kiume) au VAMIR(kwa jini wa kike). Kisha andika AL AMANI(yaani awe wa amani). Mwisho aina ya jini kama vile.
*MAJIRR AL AMAR(huyu ana nguvu sana), * AL AMAR(huyu ni wa pili kwa nguvu). *SUL AL AMAR(ana nguvu za wastani) au CLOSUN ONTEI(ana nguvu dhaifu).

6. Ukimaliza kuandika tu maneno hayo ktk kioo JINNI atakuwa ktk chumba chako na utaona kama kuna mtu vile lakini hutomwona. Utahisi harufu ya manukato, kupumua na sense kama kutembea nk.

7. Mwamrishe aingie ktk pete au mkufu ulioandaa kwa kusema maneno haya "EWE JINI NAKUAMURU UINGIE KTK PETE/MKUFU HUU". Kisha nyofoa nywele yako moja ya kichwami na uichome kidogo kidogo ktk mishumaa yako inayoendelea kuwaka kwa dk. 1-2.

8. Mfungie ktk pete kwa kusema mara 3 maneno haya "EN TIEN ALLAH CLMAN".

9. Zima mishumaa yako kwa kuanzia mwekundu, mweusi kisha mweupe. Futa maneno uliyoandika ktk kioog.

Hapo pete yako au mkufu wako utakuwa na JINNI na namna ya kumtumia nitawajuza baadaye ngoja nipate kwanza lunch.

ITAENDELEA...............

========
PART 2:
Quote By Mcheza Karate View Post
Ni mwendelezo wa mada yetu ya juzi ya jinsi ya kuita JINI na kumtumia.

Nianze kwa kujibu maswali na tuhuma kabla sijaendelea.

MASWALI.

1. Kwa nini maneno yaliyotumika hapo ni ya QURAN? Je Quran na majini kuna uhusiano gani?
Jibu: maneno yanayotumika kuita hawa viumbe sio ya quran bali ni ya kiarabu. Kuna tofauti kubwa kati ya kiarabu na quran. QURAN ni Kikureshi, ni lahaja ya Kiarabu. Hivyo hata waarabu wasio wakureshi hujifunza Quran.

2. Kwa nini majina ya waislamu hutumiwa na majini?
Jibu: Chanzo cha wanadamu na ulimwengu wa kiroho ni mashariki ya kati, hivyo idadi kubwa ya jamii ya waishio mashariki ya kati ni waarabu, haiyumkini kujenga hoja hii ni udhaifu. Vilevile kuna majini kama DAIMON huzungumza kiingereza na kijerumani hivyo kusema wapo majini wanaozungumza lugha tofauti na kiarabu.

3. Mwisho kuna walionidhihaki kuwa natangaza ushetani, na mimi ni mganga wa jadi.
JIBU:Si kweli, msingi uliopo ni kuwa tuko ktk mitandao ya kijamii na tunajadili mambo mbalimbali. Mimi natoa experience na mada ya kitu nilichofanyia uchunguzi/reseach kwa miaka 4 na ktk nchi 5, ukiona ni ushetani ni hulka yako. Ukiona kusoma neno Jini unadhurika nenda ktk quran au bible yako kafute sehemu zote zilizoandikwa JINI. Ha! ha! ha! ha! ha!

MWENDELEZO WA MADA YETU.

JINSI YA KUMTUMIA JINI TULIYEMWITA.
Matumizi ni ya aina mbalimbali kama vile unavyotaka taarifa kwa kugoogle ktk mtandao.

1. Unataka kuwa mahusiano ya kimapenzi na jini uliyemwita.cha kufanya ni kumwomba kwa maneno kama haya kabla ya kulala "WEWE JINI NAKUOMBA LEO TUSHIRIKIANE KTK TENDO LA ***". Usiku utaota unafanya tendo na binti mrembo/mvulana handsome na ukishtuka utakuta tayari umechafuka. Angalia na jinsia ya jini uliyemwita. Isije wewe ME umemwita MUSCHNA halafu unamwomba mDO.

1. Unataka kumtumia kwa ajili ya kupata pesa na mafanikio. Ni rahisi tu. Chukua karatasi isiyoandikwa then andika "ni biashara gani nifanye na kuniletea mafanikio na je unaweza kunisaidia ni wapi naweza kupata pesa ya mtaji?" halafu fumba macho na weka kalamu yako chini kidogo ya hiyo sentensi na uanze kuandika kama mtoto wa chekechea, usikusudie kuandika wala kuumba herufi(nadhani uumenipata), dont consider what you are writing. Baada ya kufanya zoezi hili kwa dk. 1-3 fumbua macho. Utaona maelezo aliyokupatia kuhusu mnyambuo wa biashara pamoja na wapi kwa kupata mtaji kwa msaada wake. Mf.Akikuambia nenda kamkope flani usisite, walah anakupatia kiasi chote unachohitaji.

Kwa kweli ni kama kutafuta kitu kwenye mtandao vile. Chochote ambacho undahitaji anakusaidia.

TAHADHARI.

-Usimwite JINI kisha kabla ya kumaliza hatua zote ukakimbia kwa woga nk.
-Usimwite jini MAJIRR AL AMAR kama ni mara yako ya kwanza.
-Usinywe pombe siku ya kumwita JINI.

ALAMSIKI!!!

PART 3:
Quote By Mcheza Karate View Post
Salaam,

Tumepotezana kitambo hapa, ni majukumu tu ndo yanatatiza.

Leo nakuja kuwaletea elimu mbadala juu ya kudumisha na kuboresha mahusiano yako ya mapenzi, sehemu ya kazi, ktk sehemu unayoishi nk.

NOTE: Hii itakufanya upendwe na watu, mpenzi au kazini isivyo kawaida hivyo kukuongezea nafasi ya kusonga mbele.

MAHITAJI

1. Chumba safi na kitulivu.
2. Mishumaa(white candles) mitatu au saba.
3. Karatasi nyeupe(A4) zisizochorwa mistari.
4. Kalamu nyekundu 1
5. Uwe tayari umeandaa hitaji lako kama la kujenga mahusiano kazini, kupendwa, kuogopwa na watu au jamii unayoishi nayo.
6. Kiberiti.
7. Udi[njiti 3)

MUDA

-saa 6:55(saa sita na dakika hamsini na tano usiku)
-siku za jumapili, jumanne na alhamisi ni nzuri zaidi.

HATUA

Kutokana na muda na "kamchina" ninakotumia kupost hapa naomba niendelee kuelezea hatua na nini cha kufanya panapo kesho.


Jinsi ya kumwita jini na kumuamrisha unavyotaka. Awe rafiki, mpenzi au msaidizi Jinsi ya kumwita jini na kumuamrisha unavyotaka. Awe rafiki, mpenzi au msaidizi Reviewed by CapchaMuzic on 22:08:00 Rating: 5
Powered by Blogger.