Hatari kwa Usalama wetu!!Mwanajeshi Alewa Chakali na Kulala katika Mfereji wa Maji Machafu
KATIKA
hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT)
anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada
ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo
la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa
Tukio
hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha
askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka
Mafinga kuja mjini Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa wa
askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya
wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa
askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote
wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na
kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.
Hata
hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo
kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla
ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .
Alisema
kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake
ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na
kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima
jeshi kwa ulevi uliopitiliza
Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya
mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo
sana mambi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na
kumpeleka eneo la Kihesa .
Ushauri wetu kwa askari wetu
kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe
ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama
chonde chonde ulevi noma.
Hatari kwa Usalama wetu!!Mwanajeshi Alewa Chakali na Kulala katika Mfereji wa Maji Machafu
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:42:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:42:00
Rating: