Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni
Nianze
kwa kukuuliza wewe mzazi; unapoweka picha ya mtoto wako kila hatua
tangu akiwa mchanga hadi anaanza kutembea na kuanza shule, alikuomba au
ulipata ruhusa yake?
Ingekuwa wewe umepigwa picha bila idhini yako halafu ukaikuta kwenye mtandao utafurahi?
Najua
unampenda mtoto wako na ana haki zake za msingi pamoja na kuheshimiwa
faragha yake popote alipo. Haiwezekani chochote anachofanya ukiweke
kwenye mtandao.
Naomba
kueleza madhara yanayoweza kutokea kwa kuweka picha za mtoto wako au wa
mwenzako kwenye mitandao hasa mitandao ya kijamii kama facebook ,
instagram na mingineyo.
Kwanza
fahamu kuwa kampuni karibu zote za mitandao ya kijamii zimesajiliwa
Marekani, chache zimesajiliwa Ulaya na Asia, lakini karibu zote
zinatumia sheria na sera za mataifa hayo.
Katika
mataifa hayo wanasisitiza mtoto asijiunge kwenye mitandao ya kijamii
hadi atakapofikisha miaka 13, wengine miaka 15 au 16 .
Kampuni
zote za mawasiliano zina utaratibu wa kuhifadhi kila kitu kinachotokea
kwenye shughuli zao za kila siku kwenye chombo maalumu cha kuhifadhi
taarifa za mtandao (server). Kwa hiyo ukiweka picha za mtoto
zinahifadhiwa huko hata kama utazifuta.
Hapo
awali, nilisema mtoto anahitaji faragha yake, unaporusha picha za mtoto
wako kwenye hii mitandao au mawasiliano yoyote, unaingilia faragha yake
na huko mbele anaweza kukushtaki wewe au wengine walioingilia faragha
yake.
Mtoto
anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha
kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye
mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano .
Umeshawahi
kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu
kwenye mitandao hasa ya kijamii ? unajua ni kwa nini ?
Kwa
sababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa
karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na
ndugu zake.
Kama
ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na ‘mabazazi’ kwa sababu ya
picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja
akabakwa.
Kwa hisani ya mwananchi tunapata elimu
Hoja yangu:
Kwanini
hii tabia imezuka sana wanandoa siku hiyo hiyo mama anaugulia maumivu
badala ya baba kumhangaikia mama na mwanae yeye anafuta kamera iko wapi
tena siku hizi mchina amerahisisha anamfotoa mtoto na kupost kwenye wall
yake ili iweje? kwamba watu wajue na wewe ni kudume cha mbegu au una
kizazi? matokeo yake ndo wazazi mnapotofautiana na marafiki zenu
mnawatukana mpaka watoto, kuna wengne sijui mtandao gani yule dada
anauza pichu anamtukana mtoto wa mwenzaje eti baboon hivi mnahisi watoto
wanajisikiaje? unamharibia mtoto future yake bila kujua, ukifikiri ni
fahari kuweka picha ya mwanao sijui facebook, twitter, instagarma na
kwingne huko ni ushamba na ujinga, labda siku hizi kwa kuwa imekuwa
issue sana kupata mtoto but is not fair
Nawasilisha hoja
Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:53:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:53:00
Rating: