Ney wa Mitego aongelea tetesi zilizo zagaa za yeye kuwa Freemason
Video mpya ya ‘Mr Nay’ imemfanya Nay Wa Mitego kuwa na kazi ya kujibu
maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali wanaomuuliza maana ya kile
kinaachoonekana kwenye video hiyo. Miongoni mwa maswali hayo tayari ameyatolea majibu, ikiwa ni pamoja na maana ya idea ya video hiyo ambayo Nay mwenyewe alisema ni wazo tu alilipata lakini hajui ina maana gani.
Swali
lingine ambalo Nay Wa Mitego amelitolea ufafanuzi ni,”Zile damu, na
vitu vingine kama vya kishetani pamoja na namba ninayopenda kuitumia ya
#966 ni vitu vinavyofanya nipate sana msg na kuulizwa maswali”, alisema
Nay alipozungumza na Millard Ayo.
Kuwaondoa hofu wale walioanza kupata wasiwasi kutokana na video hiyo ikiwa ni pamoja na mama yake mzazi, Nay amesema:
“na ndivyo vitu vimemshtua mama mpaka akaniita, watu wengine wanadhani
mimi ni mwabudu shetani ila nataka watu watambue kwamba hakuna kitu kama
hicho, ni ubunifu tu”.
Video ya ‘Mr Nay’ imefanyika nchini Kenya na kuongozwa na Kevin Bosco Jnr.
Ney wa Mitego aongelea tetesi zilizo zagaa za yeye kuwa Freemason
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:31:00
Rating: