Angelina Jolie na Brad Pitt wauza picha zao za harusi kwa shilingi bilioni 3.3
Kanye West na Kim Kardashian walikataa kuuza picha zao za harusi lakini si kwa Angelina Jolie na Brad Pitt.
Mastaa
hao ambao kwa pamoja hujulikana kama Brangelina wameuza picha zao za
harusi kwa dola milioni 2, ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.3 za
Tanzania. Kiasi hicho cha fedha kimepatikana baada ya kulipwa na
majarida mawili ya People na Hello!, wiki moja baada ya kufunga ndoa
Aug. 23 nchini Ufaransa.
Hiyo
sio mara ya kwanza Pitt, 50, na Jolie, 39, wameingiza fedha kutokana na
maisha yao binafsi licha ya kuwa na maisha ya usiri. Wawili hao wala
hawana msemaji wao.
Mwaka 2006, waliuza picha za kwanza za mtoto wao wa kike, Shiloh kwa jarida la People kwa dola milioni 4.
Mwaka 2007, Jolie na Pitt walifanya kazi na People na Hello!, tena kwa
kuuza picha za kwanza za mtoto wao wa kiume, Pax kwa kiasi ambacho
hakikujulikana.
Mwaka 2008, walidaiwa kulipwa dola milioni 14 na
jarida la People kuchapisha picha za kwanza za watoto wao mapacha,
Vivienne Marcheline na Knox Leon. Kwa pamoja wawili hao wana utajiri wa
dola milioni 385.
Angelina Jolie na Brad Pitt wauza picha zao za harusi kwa shilingi bilioni 3.3
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:24:00
Rating: