MCHINA IRINGA ACHEZEA KICHAPO KWA KULAZIMISHA PENZI KWA MKE WA MTU
Mchina akichezea kichapo kwa kumshika mke wa mtu maziwa mjini Iringa
...................................................................................................
RAIA mmoja wa Kichina ambae jina lake
halikuweza kupatikana mara moja anayesadikika kuwa ni mmoja kati ya
mafundi katika ghorofa moja mjini Iringa amejikuta akichezea kichapo
kutoka kwa njemba mmoja ambae alikuwa ameongozana na mke wake baada
ya mchina huyo kumshika maziwa mwanamke huyo akimtaka mapenzi mbele
ya mumewe .
Tukio hilo lililofananishwa na
udhalilishaji kwa wanawake lilitokea jana majira ya saa 2 usiku katika
eneo la stendi ya daladala za Mkwawa kata ya Miyomboni mjini
Iringa.
Kutokana na kitendo hicho cha aibu
alichokifanya mchina huyo mume wa mwanamke huyo alikosa uvumilivu na
bila kujali kuwa wachina ni wataalam wa kareti alimvaa mchina huyo
na kumpiga mtama uliopelekea kuanguka chini na kuwafanya vijana
wapiga debe eneo hilo kuanza kumshambulia kwa kichapo bora mradi
wamepigana na mchina .
Vijana wakimpa kichapo mchina huyo |
Mashuhuda
wa tukio hilo waliueleza mtandao huu wa matukiodaima.co.tz uliofika
kwa wakati eneo la tukio kuwa mchina huyo alikuwa akitoka katika
eneo la jengo wanalolijenga lililopo jirani na stendi hiyo na baaada
ya kufika eneo hilo la Stendi alikuta watu wengi wakiwa wanasubiri
usafiri wa daladala kwenda Mkwawa na Ilala na bila aibu mchina huyo
alimsogelea mwanamke huyo ambae pembeni alikuwa na mume wake na
kumshika maziwa yake mfano wa kumtaka penzi kwa nguvu jambo ambalo
lilimfanya mwanamke huyo kupiga kelele huku mchina huyo
akimsemesha kichina ambacho hakuna aliyejua anazungumza nini zaidi ya
kutambua ishara za mikono ambazo mchina huyo alikuwa akionyesha
kuashiria kumwita .
Hapa akionyesha eneo lake la kazi
.........................................................................
Kichapo kikali alichokipata mchina
huyo ambae muda wote alikuwa akilalamika kwa kilio cha kichina
ilimfanya mmoja kati ya askari anayeendesha biashara zake eneo hilo
anayetambulika kwa jina moja la Rashid kufika kunusuru ugomvi huyo na
baada ya kutamkiwa Polisi mchina huyo alipiga magoti na kuonyesha
ishara za kutubu kosa na askari huyo alisikika akisema umefanya kosa
huwezi mshika mwanamke maziwa hadharani na kuachiwa .
Hata hivyo imedaiwa kuwa ni tabia ya
mchina huyo na wenzake wanaofanya kazi katika jengo hilo kunyanyasa
wanawake na kuwavunjia heshima zao mbele ya hadhara kiasi cha baasi
na maeneo ya pombe vidanda vya UVCCM kiasi cha kupigwa marufuku
kuingia katika baadhi ya vibanda
MCHINA IRINGA ACHEZEA KICHAPO KWA KULAZIMISHA PENZI KWA MKE WA MTU
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:59:00
Rating: