Tambwe amwaga machozi Simba, atimkia kwao

Mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Amissi Tambwe. Sweetbert Lukonge na Hans Mloli  
MAISHA ya mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Amissi Tambwe katika kikosi hicho hivi karibuni yameonekana kuwa magumu na kujikuta uso wake ukipoteza furaha kila kukicha huku akibubujikwa na machozi bila ya kutarajia.
Hali hiyo inatokana na kushindwa kung’ara katika mechi mbili za kirafiki ambazo Simba imecheza huko mjini Unguja ilikopiga kambi yake ya kujiandaa na msimu ujao.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe ambaye msimu uliopitia ndiye aliyekuwa kinara wa mabao katika kikosi cha Simba, amesema kuwa anajisikia vibaya kutokana na kushindwa kufunga bao hata moja kwenye mechi hizo mbili ambazo Simba imecheza hivi karibuni dhidi ya Kilimani City na Mafunzo.
“Hakika inaniuma sana lakini ndivyo hivyo imeshatokea, lakini Jumatatu naondoka, naenda Burundi kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania, pengine nikirudi mambo yanaweza kuwa mazuri,” alisema Tambwe.
Katika safari hiyo ya Jumatatu, Tambwe ataambatana na mchezaji mwenzake wa kikosi cha Simba aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Afad FC ya Ivory Coast, Pierre Kwizera na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu ambao wote wameitwa katika kikosi cha nchi hiyo.
Tambwe amwaga machozi Simba, atimkia kwao Tambwe amwaga machozi Simba, atimkia kwao Reviewed by CapchaMuzic on 00:41:00 Rating: 5
Powered by Blogger.