‘NIMEBEBESHWA ‘UNGA’ HADI NIMECHOKA’
Stori: Mayasa Mariwata na Rhoda Josiah
Akizungumza na wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’.
“Nililetwa Dar mwaka jana na mwanaume mmoja, aliniahidi kunitafutia kazi, niliishi naye kama mtoto wake.“Zilipita kama wiki mbili tangu aliponileta bila kuniambia nitafanya kazi gani, siku moja ndipo akanipeleka Mitaa ya Magomeni (Dar) na kuniambia nitakuwa nafanya shughuli za kuuza unga huku nikiishi nyumbani kwake na yeye ndiye bosi wangu.
“Nilishangaa sana kuona ile ndiyo kazi niliyoahidiwa kuja kuifanya Dar. Nilianza kumlilia bosi wangu anirudishe kwetu Mwanza lakini alinigomea, hata pale nilipotafuta kisingizio cha kumwambia nimemkumbuka mama yangu, aliniambia nimtumie nauli aje Dar,” alisema binti huyo akilengwalengwa na machozi.
Alisema, awali alikuwa akilipwa Sh. 3,000 kila siku kwa kupakia kwenye paketi na alipobadilishiwa kitengo na kuanza kuhesabu kete na kubebeshwa amekuwa akilipwa kiduchu, yaani Sh. 50,000 kwa mwezi.
“Hii kazi sitaki hata kuisikia,
nimeshafanya kwa mwaka mmoja sasa, sijapata faida yoyote kwani nalipwa
kiduchu huku nikiishi kwa hofu muda wote hivyo nimechoka.“Kuna kipindi
mama yangu alikuja na kufikia kwake, alimnyanyasa na kumnyima nauli ya
kurudi Mwanza. Alikuwa ananiambia kama vipi nikajiuze nipate nauli ya
mama yangu.
“Kuna wakati ananitishia maisha endapo nitatoa siri popote, jambo ambalo limenifanya nikose uhuru na amani ya maisha, ndiyo maana nimeshukuru kukutana na magazeti ya Global Publishers nitue huu mzigo.”
Katika kile kinachozidi kumtia hofu ni pale alipoambiwa siku chache zijazo ataanza kusafirisha unga nchi mbalimbali na kupata utajiri mnono jambo ambalo hataki kulisikia, kwa kuwa anaogopa kuozea jela hivyo kikubwa anachohitaji ni msaada wa nauli ya kurudi kwao Mwanza akamsaidie mama yake ambaye ni mzee na ni mgonjwa.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari ya mwanadada huyu na anahitaji kumsaidia nauli ya kumrudisha Mwanza, awasiliane nasi kwa namba 0719595558.
‘NIMEBEBESHWA ‘UNGA’ HADI NIMECHOKA’
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:39:00
Rating: