Suge Knight apigwa risasi sita katika Pre- MTV VMA Party iliyoshereheshwa na Chris Brown

Party ya utangulizi wa utoaji tuzo za video za MTV (Pre-VMA Party) iliingia dosari baada ya CEO wa zamani wa Death Row Records alikuwa mmoja kati ya watu watatu waliojeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kwa mujibu wa TMZ, machafuko hayo yalitokea nje ya club ya usiku ya 10AK magharibi mwa Hollywood majira ya saa saba na nusu usiku.
Suge Knight anaripotiwa kupigwa risasi sita zilizompata tumboni, mkononi na sehemu nyingine za mwili. Alikimbizwa hospitali ambapo hali yake inaripotiwa kutia matumaini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Polisi walifika katika club hiyo na watu wote walitoka wakiwa wameweka mikono juu kufuatia tukio hilo la hatari.
Chris Brown alikuwa mshereheshaji katika party hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Tyson Beckford.
Mashuhuda wameeleza kuwa kabla ya tukio hilo, rapper The Game na rafiki zake waligombana na mlinzi wa club hiyo na kukataliwa kuingia ndani. Game aliondoka na kuwaacha rafiki zake maeneo hayo.
Kufuatia tukio hilo,  Polisi wanafanya uchunguzi dhidi ya makundi mawili ya kihalifu ambayo yalikuwa na beef ya muda mrefu. Game na Suge Knight wote wanahusishwa na kundi maarufu la bloods.
“It's disappointing that we as a society can't have fun or enjoy ourselves without any altercations sometimes. Miss me with the bullshit!!!” Alitweet Chris Brown baada ya tukio hilo
Suge Knight apigwa risasi sita katika Pre- MTV VMA Party iliyoshereheshwa na Chris Brown Suge Knight apigwa risasi sita katika Pre- MTV VMA Party iliyoshereheshwa na Chris Brown Reviewed by Unknown on 04:42:00 Rating: 5
Powered by Blogger.