Mashosti Wawili wa Wema Sepetu Wanaomsaidia Kula Ujana Watifuana Kwa Matusi, Nusura Wazichape Nyumbani Kwa Wema
Nice Chande, Wema na Aunt |
Chanzo makini cha habari kilichokuwa nyumbani kwa Wema, kililidokeza gazeti hili kuwa waigizaji hao wakiwa na rafiki yao mwingine, walianza kutukanana kwa jambo ambalo halikuweza kubainika mara moja, huku Madam akijitahidi kuwasuluhisha bila mafanikio.
Wakiwa na dalili zote za kubugia kiburudisho cha kutosha kilichowafanya wasione vibaya kupaza sauti za matusi mbele za watu, marafiki hao walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuendelea kutukanana kana kwamba hawana akili nzuri.
Baada ya kuona watu wameanza kukusanyika usiku huo ili kushuhudia sinema hiyo, Aunt, Nice na rafiki yao walijipakiza kwenye gari, huku Aunt akiwa nyuma ya usukani na kuanza safari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake, Mwananyamala, lakini safari yao iliishia hatua chache mbele baada ya dereva huyo kulitumbukiza mtaroni gari hilo.
Kuona hivyo, watatu hao walishuka na kuanza kurudi tena nyumbani kwa Wema, ambaye aliendelea kuwasihi lakini wakiendelea kushambulia kwa maneno makali, kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa ndiye chanzo cha ajali ile.
Nyumbani kwa Wema, wasanii hao walimuomba msaidizi wake, Petit Man aende kuwasaidia kulinasua gari hilo mtaroni, kazi ambayo ilifanywa na vijana wa mtaani hapo waliolipwa kiasi cha shilingi 50,000.
Hata hivyo, baada ya gari hili kuletwa kwa Wema, si Aunt wala Nice waliokuwa tayari kulipanda, hali iliyomlazimisha mwenyeji wao kupiga simu kuita teksi, ambayo pia baada ya kufika, Nice alikataa kuipanda, badala yake Aunt na shostito wao mwingine ndiyo waliingia ndani na kutokomea.
Baada ya kukubaliana kuwa gari lile lilale hapo, Wema alimtaka Nice kuingia ndani, lakini aligoma, akidai anataka kuongea na baby wake kwa njia ya simu, lakini mwenyeji wake aliamua kuita teksi nyingine ambayo ilifika na kumchukua.
GPL
Mashosti Wawili wa Wema Sepetu Wanaomsaidia Kula Ujana Watifuana Kwa Matusi, Nusura Wazichape Nyumbani Kwa Wema
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:06:00
Rating: