kutana na aina 7 Maarufu za Libwata na jinsi zinavyotengenezwa na kazi yake

 https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcS8uDAZUw6LDOJ23ep0vbQ2xo43Rk7tsWACGKmT9dNNDI8uDc1cKw

Jamani mmeshinda poa!

Wanawake / Mabinti baadhi wamekuwa watumiaji wazuri wa limbwata kama sehemu ya kuongeza chachu ktk mahusiano yao ya mapenzi. Zifuatazo ni baadhi ya teknolojia maarufu ama niseme pendwa za limbwata. Waweza kuongeza yoyote ile uijuayo:

Kinyama

Hii kitu kuna siku Mkuu MziziMkavu aliielezea vizuri tu. Katika hili, kipande kidogo cha nyama mfano wa mnofu mmoja wa “mshikaki” huwekwa katika maku ya mtaka tiba, kwa muda wa siku kadhaa kulingana na masharti ama maelekezo ya mganga husika “fundi”, baadae kinyama hiki hupikwa na sehemu nyingine ya kitoweo kama mboga na kuliwa. Mlengwa wa limbwata ataathirika mara tu baada ya kula mlo uliohusiha mboga yenye kinyama hiki! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alielishwa kinyama

Maji ya mchele:

Hii ni aina nyingine ya teknolojia ya limbwata. Ni kwamba kwa kutumia njia hii, maji ya kawaida hupelekwa kwa mganga kwa ajili ya kazi husika, na kisha maji hayo hurudishwa nyumbani, mwanamke mhusika huyatumia maji ya dawa haya kuoshea maku na baadae huyatumia kuoshea mchele ama hata kupikia kabisa! Limbwata hili hufanya kazi kwa mlengwa baada ya mlengwa kula chakula kilichopikwa kwa maji tajwa! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alienyeshwa maji hayo, na kwamba ili kumuagua lazima apatikane fundi Yule Yule aliefanya yake!

Kisomo:

Nyingine. Hii haisemwi sana, ni kama siri kubwa, huwa haijulikani hasa ni aina gani ya “kisomo” hufanyika lakini wateja na wafuasi wa limbwata la aina hii wanakiri kuwa, mwanaume aliesomewa (msomaji ni fundi “mganga”) huwa ni zaidi ya kondoo, kwa maana ya kuwa maisha yake yote yaliyobaki yanakuwa ni yale ya “ndio mzee” kwa mwanamke alietengeneza! Wanaoipenda njia hii wanasema sio nzuri sana kwa vile fundi mwingine yoyote anaweza akafanya kisomo kinyume.

Kifaranga:

Hapa mwanamke mhitaji huagizwa na fundi kupeleka kifaranga, na mara nyingi ni cha kuku. Fundi humfanyia kazi Kifaranga huyu katika karakana yake, namna fundi anavodili na kifaranga hiki ndio ndio kazi halisi ya kumuinamisha mme ama mpenzi wa mtu, kifaranga huyu hubaki ktk himaya ya fundi kwa maisha yake yote, na namna kifaranga huyu anavolelewa na huyu fundi, na kufuata anavotaka mfugaji, ndio hivo hivo mlengwa atakavopelekwapelekwa! Njia hii inachangamoto moja kubwa, usalama na uhai wa kifaranga huwa ni tatizo, na iko subjected to frequent updates!

Jina kuning’nizwa juu ya mti:

Hii inafanana na kisomo. Tofauti ni kwamba, baada ya fundi kufanya kazi yake, huku jina la mlengwa likiwa limenuiwa, karatasi lililoandikwa jina hili (jina la mwanaume mlengwa) huenda kuning’inizwa katika moja ya mti mrefu ambao ni sharti uwe mbali na wanapoishi wapenzi ama wanandoa hao, wakati mwingine inahusisha mkoa mmoja hadi mwingine! Wanasema kusipokuwepo na upepo, mwanaume huwa mjanja mjanja, lkn upepo ukivuma kidogo tu, mwanaume huyu akili huruka na kumuwaza aliemtengeneza! Ili upone kutoka katika limbwata hili, lazima huu mti utafutwe na kikaratasi kikatwe, ndio utapona!

Kaburi la mtoto

Hapa kuna vitu hufukiwa. Kama ilivo limbwata la hapo juu, limbwata hili linahusisha madawa na majina ya mlengwa. Kaburi husika hutafutwa maeneo ya mbali sana. Madawa na majina ya mlengwa hufukiwa katika kaburi la mtoto. Hapa huponi mpaka kaburi lipatikane na kazi ifanyike hap!

Unyayo kucha ama kinywele:
Hapa kuna mchanganyiko wa ufundi unaotumika. Wapo wanaotumia mchanga wa unyayo, wapo wanaotumia kipande cha v.u.z.i, wengine hutumia hata c.h.u.p.i ya mlengwa, lakini yote kwa yote ni kwamba fundi atadili na mlengwa kutumia aina mojawapo ya nyenzo hizi! Mafundi wengi inasemekana ni wataalamu wa kuagua wahanga wa njia hii!

Kazi kwenu wapenda michepuko!
kutana na aina 7 Maarufu za Libwata na jinsi zinavyotengenezwa na kazi yake kutana na aina 7 Maarufu za Libwata na jinsi zinavyotengenezwa na kazi yake Reviewed by Unknown on 00:52:00 Rating: 5
Powered by Blogger.