Bunge la Katiba Kufuru, Wateketeza Mamilion Kwenye Kikombe cha Chai na Biskuti Licha ya Kwamba Wanapokea Posho
Gazeti la Mtanzania August 28 2014 ndio
limeripoti hii stori kuhusu Bunge la Katiba linaloendelea Dodoma,
kikubwa ni gharama mbalimbali zinazotumiwa na Wajumbe.
Wameandika bunge la katiba lateketeza
mamilioni ya fedha ambapo kikombe cha chai na biskuti au karanga
kinalipiwa shilingi elfu 10 kila siku kwa kila Mjumbe mmoja licha ya
kwamba kila Mjumbe anapokea posho ya siku ambayo ni laki mbili na elfu
30.
Kwenye sentensi ya pili wameandika,
chakula cha mchana kila Mjumbe analipiwa elfu 16 kwa siku ambapo kwa
siku hiyohiyo iendayo kwa Mungu, ni shilingi milioni 8 hulipwa kama
gharama za ukumbi wa kufanyia mikutano.
Una chochote cha kusema kutokana na hili?
Bunge la Katiba Kufuru, Wateketeza Mamilion Kwenye Kikombe cha Chai na Biskuti Licha ya Kwamba Wanapokea Posho
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:07:00
Rating: