MAHABA NIUE: PICHAZZ..CHUCHU ARINGISHIA PENZI LA RAY!
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans amedhihirisha kwamba ana mahaba niue kwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa kulinadi jina lake hadharani kwa kuvaa t-shirt iliyoandikwa; ‘Ray Kigosi’.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans akiringisha chata la msanii Mwenzake, 'Ray'.
Tukio
hilo lilichukua nafasi wikiendi iliyopita kwenye Tamasha la Usiku wa
Matumaini lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar ambapo
mwanadada huyo aliambatana na mashosti zake kushuhudia burudani tofauti
ikiwemo mechi ya timu ya Bongo Fleva na Movies anayoichezea mpenzi wa
Chuchu Hans akipozi.
Chuchu
alivaa t-shirt ya njano ambayo mgongoni ilikuwa imeandikwa Ray Kigosi
kitu ambacho hakuwahi kukifanya kabla.“Sioni tatizo kujinadi hadharani,
atakayemaindi shauri yake, nafanya kitu roho inapenda bwana sijali
maneno ya watu hata kidogo,” alifunguka Chuchu.usiku wa matumaini
2014...
MAHABA NIUE: PICHAZZ..CHUCHU ARINGISHIA PENZI LA RAY!
Reviewed by Unknown
on
01:52:00
Rating: