INADAIWA BAADA YA KAJALA KUTEMANA NA PETIT MAN KAHAMIA KWA MSANII HUYU WA BONGOFLAVA
Gossip Cop Soudy Brown kapiga stori na meneja wa Kajala ambae alikua na wawili hawa hata wiki iliyopita Tanga ambapo kazungumzia kinachoendelea kuhusu kazi mpya ya filamu ambayo inategemewa kutoka siku si nyingi ikimuhusisha Kajala na Quick Rocker, inaitwa Mbwa Mwitu.
Meneja amekanusha stori za uhusiano huo kuwepo na kusema wawili hawa wanafanya kazi tu, kwani haiwezekani watu kufanya kazi bila kuwa wapenzi?
Soudy alimuuliza uchumba wa Quick na Kajala ukojeukoje? akajibu >>> ‘nani alikwambia wana uhusiano? hamna hicho kitu… Quick tumefanya nae movie tu, hakuna biashara nyingine yoyote zaidi ya movie’
INADAIWA BAADA YA KAJALA KUTEMANA NA PETIT MAN KAHAMIA KWA MSANII HUYU WA BONGOFLAVA
Reviewed by Unknown
on
02:10:00
Rating: