ANGALIA PICHA NA VIDEO- JAMAA AKIPAMBANA NA CHATU KWA MIKONO YAKE MWENYEWE,AMENG'ATWA ZAIDI YA MARA 100
Ruben
Ramirez mwenye miaka 41 ameamua kujitolea kuingia porini huko Florida,
Marekani kupambana na nyoka wakubwa ambao walivamia eneo hilo tangu
mwaka 2000 na kula wanyama mbalimbali katika maeneo hayo.
Ramirez
ambaye ni mwenyeji wa eneo hilo ameeleza kuwa wakati anakuwa, yeye na
baba yake walikuwa wakienda porini kuangalia wanyama mbalimbali lakini
tangu chatu hao walipovamia eneo hilo hawaoni tena wanyama hao na ndio
sababu akaamua kuwapunguza.
Mwanaume
huyo hupigana mieleka na chatu hao na kuwashika wakiwa hai kisha
kuwakabidhi kwa maafisa wa wanyama pori wanaowatoa katika eneo hilo kwa
lengo la kusaidia wanyama kukua.
Ramirez
anaeleza kuwa tayari ameshang’atwa zaidi ya mara mia au elfu kadhaa na
nyoka hao wakati akipapambana nao lakini ameweza kupona kwa kuwa wengi
huwa hawana sumu.
Pamoja na hatari kubwa anayokabiliana nayo, anadai kuwa hufurahia sana kupigana mieleka na nyoka hao.
ANGALIA PICHA NA VIDEO- JAMAA AKIPAMBANA NA CHATU KWA MIKONO YAKE MWENYEWE,AMENG'ATWA ZAIDI YA MARA 100
Reviewed by Unknown
on
10:14:00
Rating: