Huyu ndo Msanii maarufu aliye amua kuchafua Kifua Kizima kwa Tattoo Mpya ya Mareemu Mangwea asema amefunga ukurasa wa kumzungumzia

Rapper M2 The P amechora tattoo mpya ya rafiki yake marehemu Albert Mangwea, na kudai kuwa tattoo hiyo ni ishara ya kufunga ukurasa wa kumzungumzia baada ya kumweka mwilini mwake.
IMG_4945
Akizungumza na Bongo5, M2 The P amesema aliwaahidi mashabiki kuwa atachora tattoo ya rafiki yake huyo ili abaki mwilini mwake milele.
“Tatoo ni deni, kwa sababu nilivyorudi kupindi kile cha msiba baada ya kusikia msiba wa mwanangu, mimi nikawaahidi watu tattoo ya kumuenzi maisha, kwa sababu alikuwa ni mtu wangu wa karibu nilikuwa na share nae vitu vingi, nikasema siwezi kumuona kwenye picha kila siku au kumzungumzia kila ninakopita, nikasema nikipata muda wa kupumzika nitapumzika nitamtafuta mtu ambae atanichora tattoo, wakutoka nje ya bongo au ndani ya bongo, kwaiyo nikatumia wiki moja kuchora tattoo, pia huu ni mwaka mmoja tangu atutoke Ngwear sikuweza kufanya kitu kipindi hicho kilichopita ila kuanzia sasa angalau nitaanza kufanya kazi zangu.”
IMG_4948
Pia M2 The P alizungumzia thamani ya tatoo ambayo amechora kwajili ya kumuenzi rafiki yake Mangwea.
“Sipendi kuongeza sifuri mbele, hii tattoo haizidi milioni 5 na haipungui milioni 2, ila siangalii nimechora kwa thamani gani, kwa sababu Ngwear ni mtu wangu kwaiyo nikaona nikamilishe ile ahadi ya tattoo ili na mimi nifanye kazi nyingine ” Alisema.
Katika hatua nyingine M2 The P amewataka watanzania wa support wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Siabonga Nkosi.
IMG_4946

Huyu ndo Msanii maarufu aliye amua kuchafua Kifua Kizima kwa Tattoo Mpya ya Mareemu Mangwea asema amefunga ukurasa wa kumzungumzia Huyu ndo Msanii maarufu aliye amua kuchafua Kifua Kizima kwa Tattoo Mpya ya Mareemu Mangwea asema amefunga ukurasa wa kumzungumzia Reviewed by Unknown on 10:02:00 Rating: 5
Powered by Blogger.