Ndege iliyobeba wanajeshi wa Marekani yalazimika kutua kwa dharura barabarani Uganda

Ikiwa hata saa 24 hazijatimia toka taarifa ya kuanguka kwa ndege nyingine ya Malaysia jana huko Ukraine, ndege nyingine ndogo imelazimika kutua kwa dharura barabarani leo (July 18) nchini Uganda.
ug
Ndege hiyo aina ya N604AR, iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Marekani, ilitua katika eneo la Kiwawu umbali wa kilomita 22 kutoka wilaya ya Mityana na kuathiri shughuli za eneo hilo.
ug2
Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, kamishna wa wilaya Joel Walusimbi, alithibitisha tukio hilo akisema rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua katikati ya barabara.
Polisi walisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe.
Ndege iliyobeba wanajeshi wa Marekani yalazimika kutua kwa dharura barabarani Uganda Ndege iliyobeba wanajeshi wa Marekani yalazimika kutua kwa dharura barabarani Uganda Reviewed by Unknown on 14:37:00 Rating: 5
Powered by Blogger.