Chagga Barbie ndiye ameziba nafasi ya Shamsa Ford kwa Nay Wa Mitego? Nay azungumza
Jimbo la mapenzi la Nay Wa Mitego liko wazi toka aachane na aliyekuwa cousin mpenzi
wake Shamsa Ford, lakini swali ni kwamba ni mrembo gani aliyerithi
nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Shamsa ambayo huenda kuna warembo wengi
wanaitamani?
Kama
unamfatilia Nay Wa Mitego kwenye akunti yake ya Instagram sina shaka
utakuwa umeanza kuona dalili za kuwa kuna mpenzi mpya ‘mteule’
anayesubiri ‘kuapishwa’ na kuwa rasmi.
Chagga Barbie sio jina geni, ndio yule aliyezitawala headlines nyingi alipokuwa mpenzi wa Prezzo, jina lake halisi ni Starlisha Tillya lakini sasa anatumia jina la Chagga Empress Instagram.
Nay
na Chagga ambaye ni Mtanzania aishiye Marekani wamekuwa wakiweka post
zinazoashiria kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao zaidi ya urafiki wa
kawaida, lakini Nay amesisitiza kuwa hawajaingia kwenye ukurasa wa
mahaba japo Nay amekiri kuwa anampenda sana Chagga Barbie.
Novemba 11, Chagga alipost video akisema anampenda Nay, na Nay aliirepost na kuandika “Love you too bby Mtag umpendae @chaggaempress @chaggaempress”.
Nay a.k.a True Boy amefunguka kuhusu yeye na Chagga,
“Naomba
tu watu wajue ni mwanamke ambaye ninampenda, nampenda the way alivyo ni
mwanamke mzuri anavutia sio vinginevyo, labda ikija ikatokea akiwa
mwanamke wangu itakuwa ni poa zaidi lakini for this time nampenda the
way alivyo” Nay ameiambia Bongo5.
Aliendelea,
“Mimi
na Shamsa tulishaachana muda mrefu tumebaki washkaji ana bwana yake
nafikiri watu wanaona kwenye page yake anampost, lakini mwisho wa siku
nafasi ikishaachwa na mtu watu watajua wataona tu dalili, for this time
sidhani kama natakiwa kuongea mengi sana nafikiri watu wataona, lakini
watu wajue kwamba Chagga ni mwakamke ambaye nampenda namkubali amekuwa
ni rafiki yangu wa karibu sana, ni mwanamke mzuri so haijafikia hatua ya
kuwa na mahusiano ya kihivyo ila ikifikia watu wataona coz tuko
karibu.” Alisema Nay.
Nay amesema kuwa yeye na Charga Empress bado hawajakutana lakini watakutana hivi karibuni.
“Nafikiri tutakutana hivi karibuni, hivi karibuni tutakuwa pamoja bado hatujaonana”.- Nay
Chagga Barbie ndiye ameziba nafasi ya Shamsa Ford kwa Nay Wa Mitego? Nay azungumza
Reviewed by CapchaMuzic
on
06:59:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
06:59:00
Rating: