Nay afunguka mara ya kwanza kuhusu ishu ya kulea mtoto asie wake. Asema haya

KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.

Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji. Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.
Nay afunguka mara ya kwanza kuhusu ishu ya kulea mtoto asie wake. Asema haya Nay afunguka mara ya kwanza kuhusu ishu ya kulea mtoto asie wake. Asema haya Reviewed by CapchaMuzic on 00:17:00 Rating: 5
Powered by Blogger.