Ndoa ya Mwanamuziki Temba Hoi, Madai ya Usaliti Yawatesa..Temba Atishia Kuuwa kwa Anayemtuhumu Kutoka na Mkewe
NDOA ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ inadaiwa kupumulia mashine kutokana na madai ya kuwepo kwa usaliti baina yao.

“Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa.
Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Ndoa ya Mwanamuziki Temba Hoi, Madai ya Usaliti Yawatesa..Temba Atishia Kuuwa kwa Anayemtuhumu Kutoka na Mkewe
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:47:00
Rating:
