Msanii Kutoka TMK Wanaume Familly,MH Temba Apandishwa KIzimbani kwa Kutishia Kuuwa

Msanii kutoka TMK Wanaume Familly,Amani James Temba a.k.a Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuuwa kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi
Kwa mujibu wa Nipashe,Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.Mh Temba alifikishwa mahakamani hapo mapema saa 3;00 asubuhi huku akiwa amefugwa pingu chini ya ulinzi wa Askari kanzu wa kituo cha Polisi Chang'ombe
Aliwekwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya mahakama hiyo kabla hajasomewa mashtaka yake.Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2)
(a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya makosa ya jinai
Msanii Kutoka TMK Wanaume Familly,MH Temba Apandishwa KIzimbani kwa Kutishia Kuuwa
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:07:00
Rating:
