Miaka 9 Katika Ndoa ~ Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri


Mimi nimwanamke mwenye umri wa miaka 33 mume wangu ana umri wa miaka 41.Sote ni wasomi na wafanyaazi.Tumefunga ndoa miaka tisa iliyopita  tuna mtoto mmoja ana umri wa miaka 7.Wakati tunafunga ndoa wote tulikuwa mabikra.Mimi nilikua sijawai kuwa na mpenzi na mume wangu akuwahi kua na mpenzi...
Tulianza kushiriki tendo la ndoa siku ile tulipofunga ndoa.Kwa kweli kwa ujumla maisha yetu ya ndoa ni ya furaha kwa mambo yote lakini sio ya kiunyumba

Mimi na mume wangu atujawahi kuwa mbali kikazi.Maisha yote hadi leo tuko Dar es salaam pamoja.Tulipofunga ndoa miaka ya Mwanzoni tulikua tunaweza kukutana kimwili hata mara tatu kwa mwezi,miaka ilivyokua inazidi kwenda ikawa kukutana kimwili unakua mara moja kila baada ya miezi miwili na tukikutana ni bao moja tu

Sasa hali imezidi kua mbaya kwani sasa imepita miezi sita tunalala kitanda kimoja mume wangu ajanigusa,hali hii inanisononesha kwani natamani mtoto wa pili kwakweli atuna ugomvi wowote.Mimi na mume wangu wote ni wcha Mungu.

Mume wangu ni mchapakazi sana tukitoka kazini tuko wote si mtu wa anaependa kwenda kutembea bila familia.Jumamosi na Jumapili mara nyingi tunatoka out tukirudi home akuna kinachoendelea,anageuka ukutani analala kama mtotot hadi asubuhi,wala hata anigusi nikimsogelea hata asjtuki.

Na asubuhi tukiamka tunaenda ofisini na akifika ofisini lazima anitumie message mkewangu nakupenda sana,simuelewi na nashindwa kumuuliza maana mimi kama mwanamke naona aibu.

Kwakweli mawazo ya kutoka nje ayapo kabisa kichwani mwangu maana simjui mwanaume mwingine zaidi yake namuogopa mungu siwezi kucheat.Ila kwa haliilipofika naona bora nitengane nae niishi maisha yangu maana bila unyumba amna maana ya ndoa na nataka sana mtoto

Wadau naomba ushauri je hii ni kawaida,nifanyeje

Miaka 9 Katika Ndoa ~ Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri Miaka 9 Katika Ndoa ~ Simuelewi Mume Wangu Ajanigusa Miezi Sita Sasa Naomba Ushauri Reviewed by CapchaMuzic on 11:54:00 Rating: 5
Powered by Blogger.