WEMA SEPETU ATOKA NDUKI HUKU AKIWA AMELEWA BAADA YA POLISI KUTAKA KUMKAMATA....CHEZEA POLIS WEWE...USTAA PEMBENI
![]() |
Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo,
Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake
aliyejulikana kwa jina moja la Neema.Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
Spika na vifaa vingine vya muziki vilivyotumika katika sherehe hiyo vikiwekwa kizuizini.
Polisi akisimamia zoezi hilo kwa kuwawajibisha wahusika (mmiliki wa muziki na mwenye sherehe).
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) akichukuliwa kwenye bajaji.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake
halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao
katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili ya hatua za kisheria,”
alisema.
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa,
alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo
pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye
sherehe hiyo.Imeandikwa na Gladness Mallya, Musa Mateja na Hamida Hassan.
WEMA SEPETU ATOKA NDUKI HUKU AKIWA AMELEWA BAADA YA POLISI KUTAKA KUMKAMATA....CHEZEA POLIS WEWE...USTAA PEMBENI
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:42:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:42:00
Rating:
