January Makamba: Enzi za ushindi wa CCM Zimepita
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha
kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka
wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote
yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa
asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma.
Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha
kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama
vingi vya siasa kuanza kuimarika.
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa
yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka
2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka
asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.
January Makamba: Enzi za ushindi wa CCM Zimepita
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:43:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:43:00
Rating:
