Diamond Azihirisha Kwamba yeye ni Rijali , Ampa Zari Ujauzito ,Wema, Jokate na Penny Mpo?
Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib Abdul –
Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies
aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa,
HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza kudokezwa
juu ya ujauzito alionao mwanadada ZARI ambao ni fika utakuwa wa kijana
huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata wapi” ambao wachunguziwa mambo
wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake maarufu wa zamani.
USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema “I can not wait to have
you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka
kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku akiambatanisha na picha ya Ultra
sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui Ultra sound ni nini Tafadhali
google) na baadaye Zari naye akapost picha yake akichukuliwa vipimo
hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha wananchi wakimwagika na
comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika zinaonesha wawil hao
wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu
Je unafikiri hii inaweza kuwa “Project nyingine” au ni kweli wawili hawa wanatarajiwa kuwa wazazi?? Tupe maoni yako
Diamond Azihirisha Kwamba yeye ni Rijali , Ampa Zari Ujauzito ,Wema, Jokate na Penny Mpo?
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:19:00
Rating: