Lowassa alazwa Ujerumani, afanyiwa upasuaji mkubwa...
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa yako nchini Ujerumani kwa matibabu, imefahamika.
Lowassa ambae wakati wote wa kikao cha bunge hasa kipindi cha
majadiliano ya taarifa ya PAC hakuwepo Bungeni, amekuwa Ujerumani ambako
amefanyiwa upasuaji wa Kongosho.
Taarifa kutoka ndani ya familia zinadai kuwa hali ya Lowassa si mbaya sana lakini pia bado haijaimarika.
Haijaweza kufahamika mara moja kama upasuaji huo ulifanikiwa kumaliza tatizo au la.
Taarifa za kuugua kwa Lowassa zimefanywa siri kubwa ili kutowakatisha
tamaa wafuasi wanaomuunga mkono katika mbio zake za urais 2015.
Lowassa alazwa Ujerumani, afanyiwa upasuaji mkubwa...
Reviewed by CapchaMuzic
on
09:24:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
09:24:00
Rating: