WEMA SEPETU BAADA YA KUBWAGANA NA DIAMOND.. SASA YADAIWA KUTOKA NA MMASAI...POSA YAPELEKWA NA BODA BODA...USHIHIDI HUU HAPA:
GOOD
news? Habari mpya kutoka kwa mlimbwende asiyechuja Bongo, Wema Isaac
Sepetu ‘Madam au Beautiful Onyinye’ ni kwamba, Mmasai wa Kigoma, Ayoub
Nyembo ‘Masai’ ameibuka na kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi
wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda
mzima.
Mtu wa
karibu na Masai alilipenyezea gazeti hili habari kuwa, baada ya habari
za Wema kummwaga mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuandikwa
magazetini hivi karibuni, fasta Masai aliiona fursa ‘u-single’ kwa Wema,
akatangaza nia ya kumposa kwani alikuwa akimzimia muda mrefu.
“Masai
ametumia fursa, hakutaka kuchelewa maana wazo alikuwa nalo kitambo
lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kumhofia Diamond,” alisema mtu huyo.
AKUTANISHWA NA IJUMAA WIKIENDA
Baada
ya mtu huyo wa karibu na Masai kupata mawasiliano ya Ijumaa Wikienda
kisha alikutanishwa nalo maeneo ya Mwenge jijini Dar akiwa tayari
‘amejikoki’, mkononi akiwa na barua ya uchumba sambamba na bahasha yenye
shilingi elfu hamsini kama posa.
Ijumaa Wikienda: Unataka kumuoa Wema kweli au unazingua?
Masai: Nipo ‘serious’ ndiyo maana unaona nimekuja kwako nikiwa kamili na mshenga wangu nipeleke kwa mama Wema.
SAFARI KWA MAMA WEMA
Huku
mwanahabari wetu akigonga picha za kumwaga kwa kila hatua, alimwelekeza
Masai huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva nyumbani kwa mama Wema,
Mariam Sepetu ‘Mkwe’ ambapo waliambatana na mshenga wake lakini
walipokaribia, Masai alikaa sehemu na kumtuma mshenga azame ndani.
NDANI KWA MZAA CHEMA
Mshenga
alipozama ndani, alikutana na mfanyakazi wa ndani (house girl) ambaye
alipokea barua hiyo ya uchumba na kumpelekea moja kwa moja mama Wema.
BARUA YASOMWA
Baada ya kutua
mikononi mwa mama Wema, aliisoma barua ya uchumba kisha akamuomba
mshenga kuingia ndani huku akiwa na furaha hususan pale alipogundua kuwa
mkwewe mtarajiwa (Masai) ni mtu wa Kigoma.
MAZUNGUMZO YA FURAHA
“Kwa hiyo Wema wangu anatakiwa aolewe Kigoma akale migebuka eeh?,” mama alimuuliza mshenga.
Bila hiyana mshenga akajibu: “Ndiyo mama, Masai anaishi Kigoma ila ana nyumba zake Dar, huwa anakuja mara kwa mara kwenye biashara zake na pia ana mji Singida katika Kijiji cha Ikungi na ni mfugaji mzuri, ng’ombe anao wa kutosha.”
Shangwe zaidi iliongezeka kwa mama Wema baada ya kusikia Masai huyo ana mji Singida tena kwenye kijiji ambacho yeye anatokea akatoa masharti kuwa afuate taratibu za Kitanzania kwa kumtaka Masai azungumze na Wema kisha ampigie simu ndiyo apokee barua kwa amani.
HUYU HAPA MAMA WEMA
“Hili ni
jambo la kheri jamani, nimekuelewa lakini uchukue barua hii sambamba na
posa urudi kwanza ukamwambie huyo mkwe mtarajiwa azungumze na Wema
wakikubaliana, Wema yeye ndiye aniambie siku ya ninyi kuja kutoa posa
ili na mimi nijiandae,” alisema mama Wema.
Credits:Globalpublishers
WEMA SEPETU BAADA YA KUBWAGANA NA DIAMOND.. SASA YADAIWA KUTOKA NA MMASAI...POSA YAPELEKWA NA BODA BODA...USHIHIDI HUU HAPA:
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:00:00
Rating: