Nimebeba zigo ambalo sikujua hii ndio hatima yake..Kila Ninae Mfanyia Jema Anataka Kunilipa kwa Penzi
Nina
mchumba wangu anasoma chuo kikuu fulani hapa mjini, nimekuwa mshauri
mzuri sana katika mswala yake mbali mbali, kwa kiasi kikubwa nimekuwa
nikimudu hili jukumu mambo mengi niliomshauri amefanikiwa.
Kama
kawaida ya akinadada sijui ni wote au badhi lakini wengi huwa
wanakatabia haka kusifia mpenzi kwa mashoga, hapo ndo kizaa zaa kilipo
anzia. Baada ya kunifisia kwa mwezake mimi ni mzuri kwenye maswala ya
ushauri.
Basi kama ilivyo kawaida kila mazingira yana
changamoto zake, hapo ndio uwezo wa mtu huwa unaonekana jinsi anavyo
weza kukabiliana na matatizo,,kwenye hili wenzetu huwa linawapa shida
kiasi fulani wanayokumbana nayo nimengi.
Masimulizi ya
mchumba wangu yaliwafanya kuwa na hamasa ya kutaka kunijua na kupata
mawasiliano yangu, ilitokea siku moja rafiki wa mchumba wangu akawa na
tatizo fulani akamuomba anihusishe na mimi iliniweze kumpa ushauri, bila
hiana nilishiriki tukafanikiwa katika hilo.
Sifa ikazidi kuenea kwa wengine ambao hawakunifahamu, nikawa nawashauri kimasomo na maisha mengine ya kichuo.
Wengi
wao walivutiwa na kazi yangu ya ushauri, mambo yao mengi wakawa
wananihusisha na mimi bila kusita kiwa nawasaidia, hayo yote yalikuwa
yakifanyika kwa njia ya simu, nilijizuia kujenga mazingira ya kuonana
nao sababu nilijua vishawishi ni vingi na mganga hajigangi.
Matokeo
ya hayo yote yamegeuka kuwa zigo mchezo sasa umebadirika, ili shem
haizingatiwi majina ninayopewa ni yanaleta vishawishi ya kuchepuka kama
hauna uvumilivu, maana wanajenga mazingira ya kuninasa kila mmoja kwa
wakati wake pasipo kujua, kwenye hili hawatanipata sioni sababu ya
kumsaliti mpenzi wangu na sitaki ajue nitazua chuki kati yao.
Jamani hivi malipo ya kutenda jambo jema kwa mtoto wakike lazima akulipe mapenzi ndo aridhike?
Sio
mara ya kwanza kusikia haya mambo kwamba mara nyingi mtoto wa kike ili
aridhike unapomtendea jambo la kumfura hisha anajisikia faraja akikulipa
kwa mapenzi. (Nisipigwe jiwe nasikia sikia na mimi ni tetesi sijui kama
ni kweli)
Ila nashukuru mizinga hawajanipiga maana kwenye hili nalo nasikia hawajambo.
Nimebeba zigo ambalo sikujua hii ndio hatima yake..Kila Ninae Mfanyia Jema Anataka Kunilipa kwa Penzi
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:15:00
Rating: