Pinda, Werema na Muhongo wataka zigo la Escrow abebeshwe Kikwete!
Dodoma kumekucha. Naomba kwa ufupi niwafahamishe kinachojiri maeneo haya (nimepiga kambi huku).
Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa anataka PM Pinda
atoke kwa sababu mbili, moja ili njia ya kupata Urais iwe nyeupe lakini
pili ili asiwe PM peke yake aliyewahi kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa.
Watu wake Edward wanahangaika sana kushawishi watu ili azma hii itimie.
PILI:
Membe naye anataka PM
ang'oke kwa sababu kuu mbili, moja ili njia ya Urais iwe rahisi lakini
pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM japo kwa muda tu ili
nyota ing'are zaidi.
TATU:
Wassira naye anatakaPinda aanguke ili njia iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM.
Mwandosya naye anataka PM adondoke kwa matumaini ya kupata uPM kutokana na utu uzima.
Sitta naye vivyo hivyo.
NNE:
Mawaziri walioondolewa
huko nyuma wakiongozwa na Kagasheki, Nchimbi na Maige nao wanaomba
Serikali idondoke kwa sababu wanaamini Pinda aliwatosa ili apone yeye na
sasa wanataka na yeye awajibike kwa udhaifu wake. Yupo mtu kama Mwigulu
ambaye anautaka Uwaziri kamili kwa udi na uvumba na anataka Serikali
ianguke ili Baraza la Mawaziri lisukwe upya awe Waziri kamili.
Kambi za Urais za wazee zimeungana kutaka Pinda ang'oke!
TANO:
Kwa upande mwingine hii ni vita ya watu wa Mara: Maswi, Muhongo, Werema na Mkono.
Upande mwingine ni vita ya baina ya vizazi; kizazi cha vijana na kizazi cha wazee.
Tazama Vijana walioshikilia bango suala hili ni wabunge vijana: Zitto, Kafulila, Filikunjombe, Serukamba, Mpina, Bulaya, Kigwangalla n.k.
Wanaotetea ni watu wazima: Pinda, Muhongo, Werema na wengine.
Lakini pia kwa Upande mwingine ni vita ya pesa: Kila upande umekula na ujanja ni kuwahi kupaka matope wengine!
SITA:
Kamati ya PAC imeandika
ripoti nzito zaidi ya ripoti ya CAG ambayo ni laini mno (nimebahatika
kuziona walau zote mbili). PAC, chini ya Zitto na Filikunjombe wanaweza
kuwa wamefanikisha kufanya ripoti yao iwe vizuri hivyo kwa sababu
wamewahoji watu na kupata taarifa za ziada (ambazo zitaibua mjadala
mzito sana Bungeni).
SABA:
Pinda anapigana kufa na
kupona ili apone. Pinda akianguka hapa Urais ndio kwisha. Hata hivyo,
Pinda hata asipotoka uPM atakuwa tayari amechafuka na udhaifu wake
umebainika. Ijapokuwa Wabunge wanaweza kumponya tu Pinda kwa sababu ya
kumsaidia Kikwete lakini tayari ana doa!
Hata hivyo, katika harakati za kupona Pinda, Werema na Muhongo wamekuwa wanawaambia wabunge kwamba kulikuwa na agizo la Rais la pesa kulipwa. Yaani Pinda yuko tayari kumuingiza Rais kwenye tope kulinda vyeo vyao!
Kikwete inabidi afanye maamuzi ya Kiurais, watu aliowaamini hawana hiyana kumtosa. Akimaliza Urais ndio hatari zaidi (mtakumbuka kauli yangu 2016/2017)
Pinda, Werema na Muhongo wataka zigo la Escrow abebeshwe Kikwete!
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:57:00
Rating: