Jamaa zangu wengi sana wanapata taabu sana kwa sababu ya simu. Kidude hiki ambacho kinatakiwa kitupunguzie shida katika maisha chenyewe ndio kimekuwa shida kubwa. Mtu unakuwa huna raha kabisa shauri ya kidude hiki why? Jamani Why? Kuna hii ishu ya kuwa na mchepuko, kimsingi hili jambo gumu kumalizika , kwa hiyo sihangaiki kuwambia watu waache, huko ni sawa na kukataza jua lisizame, na pia hayanihusu.

Mtu anakuwa na mchepuko wake, na sijui kwa nini michepuko ina tabia ya kuwa haina taimingi, pale mazahaus ndo uko nae, mchepuko ndo unapiga simu.
Ili kukwepa maswali watu wanaweka simu kwenye silent, wengine vibration, chondechonde usiweke kwenye vibration, mazahaus wote wana machale kishenzi, lazima utasikia ‘nani huyo? mbona hupokei?’
Maswali ya hatari sana usikubali yakutokee, hivyo daima weka simu kwenye silent. Japo tatizo la michepuko mingine usipopokea ndio haachi kupiga.


Ukiwa na mchepuko we sevu jina lake mjomba, au shangazi au ba mdogo, usiandike fundi majeneza au fundi pikipiki, imeshapitwa na wakati hiyo, utastukiwa. Ni vizuri kufanya mazoezi ya kuekti kwenye kioo ili wakati unasema uongo uso uwe umetulia kabisa wakati unajibu uongo, maana unaweza kulazimika kupokea simu ya mchepuko, mazahaus yuko mbele yako, ikalazimika uanzishe kujibu simu za kujidai unaongea biashara ya kuondoa kontena lililokwama, hapo lazima uekti vizuri kuliko msanii wa Bongomuvi.
Ili kupunguza mitihani hii, jamaa yangu mmoja wa Tabata amempangia mchepuko muda wa kupiga simu hii imemuondolea adha ya kulazimika kupokelea simu chooni na bafuni.
Kwa hiyo tafadhali wandugu tena chonde sana yale mnayochati futeni, hata kama lilikuwa neno tamu kama I love you my Chocolate futa usitake sifa, au litakukosti ohoo.

Amri kuu ya simu ukiwa na mchepuko ni kuwa unatakiwa kuibeba popote utakapokuwa, bafuni chooni, msibani harusini, usingizini, ukimuachia nafasi mazahaus aibebe umekwisha. Pia kama una mchepuko, ni muhimu sana umpe semina na warsha na kongamano mchepuko wako kuhusu nini cha kusema ikiwa kwa bahati mbaya simu ikiangukia mikononi mwa mazahaus. Asianze samahani nimekosea namba, hiyo imepitwa na wakati.
Yeye cha kufanya ni kuongea kwa konfidence kabisa na kuulizia kwanini hujakamilisha ripoti ya kazi, au kama we ni fundi gereji aulize gari lake mbona breki na taa hazifanyi kazi, au kama wewe ni dokta aombe ushauri kuhusu dawa ya pumu kwa ajili ya bibi yake aliyeko kijijini. Kikubwa asipaniki.
Habari ndio hiyo kazi kwako.