Harambee ya CHADEMA 'yamezwa vibaya' na harambee ya Pinda!
Wakati CHADEMA wanafanya harambee yako ya kuzindua "CHADEMA Mtandao", mhe Pinda nae alikuwa akifanya harambee ambayo yake ilikuwa ikienda kwa jina la "Changia Dawati Mashuleni"!
Katika Harambee ya mhe Pinda, ambae pia ni waziri mkuu wa JMT aliweza kupata makusanyo ya haraka kutoka kwa wafuatao:
1. Dr. Mengi alitoa kiasi cha Tshs. 100 milioni2. Mhe. Wassira alitoa kiasi cha Tshs. 20 milioni3. Mhe. Abood alitoa kiasi cha Tshs. 50 milioni4. Mhe. Mohamed Dewji alitoa kiasi cha Tshs. 100 milioniWananchi wengine pia walikuwa wakiendelea kumimina michango yao kwa wingi kwenye harambee ya kuchangia madawati.
Mpaka Harambee ya mhe. Pinda inafungwa, kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 milioni kiliwezwa kukusanywa kwa muda wa lisaa limoja tu!
Lakini wakati huo huo mpaka CHADEMA wanafunga Harambee yao, ni kiasi cha Tshs 4 milioni tu ndicho kilichokusanywa! Hii ni kwa mujibu wa Mhe. Mbowe.
Sasa ndugu Mtanzania naamini utakuwa umepata picha ya ni mambo gani ya msingi unapaswa kuyapa kipaumbele na yapi ya kipuuzi unapaswa kuyapuuza kwa kuangalia tu namna ambavyo zoezi zima la kuchangia Harambee hizo mbili, yaani: "Harambee changia Dawati mashuleni" VS "CHADEMA mtandao".
Harambee ya CHADEMA 'yamezwa vibaya' na harambee ya Pinda!
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:53:00
Rating: