Taarifa Kuhusu Wanajeshi na Polisi Kurushiana risasa huko Tarime
Hii
ni taarifa kutoka Tarime mkoani Mara ambako watu 12 wamejeruhiwa wakati
wa mashambulizi ya kurushiana risasi kati ya askari wa JWTZ kituo cha
Nyandoto na polisi wa kituo cha stendi.
Mashambuliazi hayo ya kurushiana risasi na kupigana ngumi na mateke
yalitokea juzi jioni katika kituo hicho cha stendi ambapo Mganga
Mfawidhi Hospitali ya Tarime alithibitisha kupokea majeruhi 12 na kati
yao wawili ni askari wa JWTZ, Polisi saba na raia watatu.
Kamanda wa Polisi Tarime alisema Mwanajeshi huyo licha ya kukiuka
taratibu za barabarani aliwatolea lugha za matusi polisi hao jambo
lililowalazimu kumkamata kwa nguvu na wanajeshi wenzake kuingilia kati
na kusababisha vurugu.
Alisema Wanajeshi watatu ambao hawakutajwa majina wameshikiliwa na
polisi kwa kuvunja utaratibu wa usalama huku Mkuu wa Wilaya hiyo John
Henjewele akilaani kitendo hicho cha kurushiana risasi za moto hewani na
kusema ni cha utovu wa nidhamu na kilikwamisha shughuli za watu kwa
muda sababu ya kuhofia usalama wao.
Taarifa Kuhusu Wanajeshi na Polisi Kurushiana risasa huko Tarime
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:03:00
Rating: