DUH!BINTI WA MIAKA 15 ACHANJWA NA VIWEMBE NA WENZAKE ILI KUHARIBU UZURI KWANI WANAUME WALIKUWA WANAMPENDA SANA

Binti
mdogo wa miaka 15 raia wa Argentina Julia Alvarez amepatwa na majanga
yaliyomfanya apoteze muonekano wake mzuri baada ya mabinti wawili wenye
wivu kumcharanga uso wake kwa visu kisa uzuri wake uliopitiliza!Julia
anasema alikuwa anatembea kurudi nyumbani akitokea mji wa Juan Domingo
Peron huko northern Argentinian ndipo wasichana hao wawili mmoja ana
miaka 18 na mwingine 16 walipomvaa bila huruma.
"Kila
mtu anasema wewe ni mzuri sana..huwezi kuonekena mzuri tena
tukishamalizana na wewe hapa..na watu watakuita majina mabaya'' Julia
alisema haya ni maneno aliyoambiwa kabla ya kucharangwa visu usoni.

Hili ni eneo ambalo tukio hilo la kikatili lilipofanyika .
Kupitia ukurasa wa facebook dada wa Julia aliandika ;
"Walikuwa
wanamuonea wivu sana mdogo wangu na kila mara wamekuwa wakimsumbua
lakini sikutegemea kama wangefika mbali kiasi hiki. Nimejaribu kuwa
imara lakini kila muda naomuona mdogo wangu nataka kudondosha
machozii...wamemuharibia maisha. Anasema anataka kujiua kwa sababu kila
akijitizama kwenye kioo anajiona mbaya sana sasa, wameharibu familia
yetu''
Polisi waliwatia mbarioni mabinti hao lakini walimuachia wa miaka 16 kutokana na umri wake ila wa miaka 18 bado wamemshikilia.
DUH!BINTI WA MIAKA 15 ACHANJWA NA VIWEMBE NA WENZAKE ILI KUHARIBU UZURI KWANI WANAUME WALIKUWA WANAMPENDA SANA
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:07:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:07:00
Rating: