Kajala ampeleka mama Wema mahakamani baada ya kumtukana matusiya nguoni, soma mkasa mzima hapa..
Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema
Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo,
mengine yameibuka!
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili
iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya
kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa
shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya
kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia
matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana
kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini
ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa
na zuio la kisheria.
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala
baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya
kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa,
timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo
yake, wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika
sana.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Katika sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki)
huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa
kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka
mama yake afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba
Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku
najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya
simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya
mwandishi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila
kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama
kumi na tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo
anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa
kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama
Wema?’
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda
alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura
Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao
wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba
mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani
hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa
mmoja.
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano
lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i
lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na
Kadinda!Chanzo: Gzeti la Amani/gpl
Kajala ampeleka mama Wema mahakamani baada ya kumtukana matusiya nguoni, soma mkasa mzima hapa..
Reviewed by CapchaMuzic
on
06:51:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
06:51:00
Rating:
