DIAMOND ACHARUKA BMW LA WEMA!
Stori: Mwandishi Wetu
Ni sheeedah!
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amecharukia gari aina ya
BMW 545 alilozawadiwa mwandani wake, Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, akipinga gari hilo
kupewa na meneja wake, Martin Kadinda.
DIAMOND ACHANGANYIKIWA
Habari za kipekepeke
zilidai kuwa, taarifa ya Kadinda kumpa zawadi ya gari Wema kwenye pati
ya bethidei yake Jumapili iliyopita, nyumbani kwake, Kijitonyama, Dar
zilimchanganya Diamond na kudai kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani kwa
maana anamfahamu vyema Kadinda kuwa hana uwezo huo wa kununua BMW la
zaidi Sh. milioni 56 za madafu.
Chanzo hicho kiliweka wazi kwamba mkali huyo anayekimbiza na Ngoma ya
Mdogomdogo alihamaki baada ya kupata taarifa kuwa siyo yeye peke yake
aliyekabidhi zawadi ya gari (Nissan Murano) kwa maana aliamini mwenye
zawadi ya gari alikuwa ni yeye tu ambayo ilikuwa ‘surprise’ kwa mpenzi
wake huyo.
BOFYA HAPA KUPATA ‘UBUYU’
“Unaambiwa Diamond
kachanganyikiwa kabisa kusikia Wema kapewa gari, tena BMW na mbaya zaidi
aliyempa gari ni Kadinda huku yeye akiamini kabisa zawadi aliyotoa kwa
mpenzi wake asingeweza kupata kwa mtu mwingine yeyote, mwenyewe anasema
amedhalilishwa kwani hawezi kutoa gari kisha mwanaume mwenzake naye atoe
gari,” kilidai chanzo hicho.
Mpashaji huyo alizidi kufafanua kwamba baada ya kupokea taarifa hizo
na kuona kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali akiwa nje ya
nchi, Diamond alianza kufanya utaratibu wa kurudi nchini akitokea Canada
ili kujua vizuri kuhusu undani wa hilo gari.
“Yaani ninyi mtasikia, nakwambia kimenuka maana Diamond aliposikia na
kusoma habari za BMW la Wema alianza kufanya utaratibu wa kurudi Bongo
ili kupata ufafanuzi zaidi,” kilisema chanzo hicho.
KADINDA AKOMAA
Kwa upande wake Kadinda ameendelea kusisitiza kwamba yeye ndiye aliyenunua gari hilo na kumkabidhi Wema ikiwa ni michango ya watu wanaomsapoti mwanadada huyo.
Kuhusu gari hilo, watu kibao wamekuwa wakitajwa kulinunua akiwemo mfanyabiashara Mkongo mwenye jina linaloanza na herufi S na mume wa mtu ambaye ni kigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar anayetajwa kwa herufi moja ya L.
Kwa upande wake Kadinda ameendelea kusisitiza kwamba yeye ndiye aliyenunua gari hilo na kumkabidhi Wema ikiwa ni michango ya watu wanaomsapoti mwanadada huyo.
Kuhusu gari hilo, watu kibao wamekuwa wakitajwa kulinunua akiwemo mfanyabiashara Mkongo mwenye jina linaloanza na herufi S na mume wa mtu ambaye ni kigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar anayetajwa kwa herufi moja ya L.
WEMA VIPI?
Jitihada za kumsikia Wema ziligonga
mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa
nyumbani kwake hakuwepo hivyo juhudi za kupata lake la moyoni
zinaendelea. Stay tuned kwani inavyoonekana nyuma ya pazia ya gari hilo
kuna siri kubwa!
DIAMOND ACHARUKA BMW LA WEMA!
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:30:00
Rating: