ZENGWE USAJILI WA FALCAO, MAN UNITED YADAIWA KUMSAJILI NJE YA MUDA
ZENGWE.
Manchester United inadaiwa kubebwa katika usajili wake, baada ya
kukiuka kanuni hususan katika usajili wa mshambuliaji Radamel Falcao.
Gazeti
la Daily Mail la Uingereza limeandika kwamba, Falcao amesajiliwa baada
ya dirisha la usajili kufungwa Saa 5:00 usiku jana- wakati beki Marcos
Rojo pamoja kusajiliwa mapema, lakini bado hajapatiwa visa ya kufanyia
kazi.
Inaelezwa Jumatatu ndiyo pazia la usajili limefungwa, lakini hadi Saa 5:00 usiku uhamisho wa Falcao ulikuwa haukamilika.
Sheria
za usajili zinasema usajili wote uwe umekamilishwa ifikapo Saa 5:00
usiku wa kufungwa pazia na baada ya hapo, vielelezo vyote kama mikataba,
makubaliano ya uhamisho na vibali vya kufanyia kazi Uingereza lazima
viwasilishwe.
Sheria imefuatwa? |
Ligi
Kuu ya England inaruhusu saa mbili, huo ni uamuzi wao – lakini uhamisho
wa kimataifa lazima uaendane na mfumo wa FIFA wa elektroniki (TMS)
kufungwa usiku huo.
Mfumo wa FIFA wa TMS ni wa mtandao ambao unatoa fursa kwa data zote muhimu kuingizwa ili kuweka sawa uhamisho wa kimataifa.
Angalau
usajili wa Rojo wa Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon umekamilika
katika masuala ya kisoka. Amepewa hati ya kimataifa na Chama cha Soka na
aliwasili England wiki iliyopita kukamilsha dili lake.
Lakini sheria za uhamiaji zinasema wachezaji wanaoingia nchini humo, lazia wawe na visa za kufanyia kazi.
Na
maofisa wa Ubalozi kwanza watafuatilia madai ya kwamba kukwama kwa visa
yake kunatokana na ugomvi baina yake na jirani yake nchini kwao,
Argentina mwaka 2010 kabla ya kumpatia visa ya kufanyia kazi, huku tukio
hilo bado linachunguzwa na Polisi.
Lakini
wakati wachezaji wa Man United wamepitishwa pamoja na kuwa nje ya muda
au kukwama kwenye baadhi ya mambo ya msingi katika usajili wao,
wachezaji wengine wamekwamishwa na hapo ndipo Daily Mail wanapouliza
haki wapi?
Usajili batili? Usajili wa Falcao inadaiwa umefanyika baada ya pazia kufungwa
ZENGWE USAJILI WA FALCAO, MAN UNITED YADAIWA KUMSAJILI NJE YA MUDA
Reviewed by CapchaMuzic
on
09:20:00
Rating: