UREMBO HUU JAMANI MMH: FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!
Katika
zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili
na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika
tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi
kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama
ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla
hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.
Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa.
Matokeo mazuri zaidi ya kutoga
ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo
mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino,
kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye
kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa
katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni
ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki.
Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya muda hutokea.
Madhara ya kutoga Ulimi
Kuvuja damu kiasi kidogo
hutarajiwa, kuna hatari ya mishipa ya damu kuharibiwa wakati wa kutoga
ulimi, hali inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa kiasi kikubwa kuliko
ilivyotarajiwa.
Ingawa kuvimba kwa ulimi
kunatarajiwa baada ya kitendo cha kutoga ulimi, wakati mwingine ulimi
huvimba kwa kiasi cha kuziba kwa njia ya hewa. Kuziba kwa njia ya hewa
kunaweza kusababisha kifo
UREMBO HUU JAMANI MMH: FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:19:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:19:00
Rating: