SHILOLE: MPENZI WANGU NDIYE ANAYENITIBU VIZURI KUNAKO SITA KWA SITA
Na Imelda Mtema
STAA
wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungua kinywa chake na kusema
mpenzi wake wa sasa, Nuh Mziwanda ndiye anayemtibu vizuri kunako ‘sita
kwa sita’ japokuwa watu wengi wamekuwa wakiudharau mwili wake.
Akizungumza na gazeti hili bila kung’ata maneno, Shilole alisema
wengi wanashindwa kujua kwamba mtu anaweza kuwa na mwanaume mwenye umbo
kubwa lakini akawa hayajui mapenzi lakini mwenye umbo dogo kama Nuh,
akawa ni bingwa wa mapenzi.
Akiendelea kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Amani, msanii huyo
anayetamba na wimbo wa Nakomaa na Jiji alisema kuwa katika mapenzi, umri
wala ukubwa wa umbo hauna maana yoyote.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
“Yaani kwa kweli Nuh ananimudu na tunaenda sawa katika suala zima la
mapenzi, kwa hiyo sioni udogo wake kwangu, kwa upande wangu Nuh ni
mkubwa sana watu wasiangalie mwili,” alisema Shilole pasipo kutaja umri
wa mpenzi wake huyo.
Shilole aliongeza kuwa, kutokana na mahaba ya nguvu anayoyapata
kutoka kwa mpenzi wake huyo, anapata nguvu ya kufanya kazi vizuri siku
hadi siku hivyo hapati tamaa.
“Sina stress za mapenzi na mara nyingi nafanya kazi zangu zinaenda sawa kabisa,” alimalizia Shilole.
SHILOLE: MPENZI WANGU NDIYE ANAYENITIBU VIZURI KUNAKO SITA KWA SITA
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:18:00
Rating: