Picha: Vazi alilovaa Angelina Jolie kwenye ndoa yake lawekwa wazi
Angelina Jolie na mumewe Brad Pitt wameweka wazi vazi alilovaa ‘bibi harusi’ katika siku ya ndoa yao iliyofanyika Ufaransa.
Picha za Angelina akiwa amevaa vazi la kwanza katika tukio hilo
zimekava jarida la People ‘PEOPLE magazine’ toleo la hivi karibuni.
Angelina Jolie ameliambia jarida hilo kuwa mbunifu wa mavazi Luigi Massi ndiye aliyemvalisha katika siku hiyo.
“Luigi ni kama familia kwangu na sikufikiria mtu mwingine yoyote wa
kunitengenezea vazi hili. Anajua na anajali kuhusu watoto na
ilifurahisha kuweka hivi vyote pamoja.” Amesema Angie.
Kwa upande wa Brad Pitt, inaelezwa kuwa alinunua suti yake katika
duka lililokuwa karibu na kuazima tai ya mtoto wao wa kiume kwa kuwa
alisahau yake nyumbani. Lol.
Pete ya ndoa ya wawili hao ilibuniwa na Robert Procop, sonara aliyetengeneza pete yao ya uchumba.
Wakizungumzia kuhusu ndoa yao hiyo iliyohudhuriwa na wageni 20 ambao
ni marafiki wao wa karibu na familia, walisema ilitawaliwa na vicheko.
“Ilikuwa muhimu kwetu kwa kuwa ilikuwa ya kujiachia na ilitawaliwa na
vicheko. Ilikuwa siku maalum ya kushare na watoto wetu na siku ya
furaha kwa familia yetu.” Walisema.
KWAPICHA ZAIDI YA HARUSI IYO BONYEZA HAPA CHINI
Picha: Vazi alilovaa Angelina Jolie kwenye ndoa yake lawekwa wazi
Reviewed by CapchaMuzic
on
04:08:00
Rating: