Mwanamitindo Hamisa Mabeto Amwanika Mpenzi Wake na Kumwagia Sifa Kede Kede
MAHABA niue! Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto
ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya
kijamii huku akimmwagia sifa kemkem.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya, Hamisa
alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya
kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon!
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye
anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa
karibu yake.
“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote
kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.
Mwanamitindo Hamisa Mabeto Amwanika Mpenzi Wake na Kumwagia Sifa Kede Kede
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:28:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:28:00
Rating:

