Martin Kadinda; Wema Sepetu Hana Pesa Ya Kunilipa, Nahangaika Ili Tusilale Njaa
Martin Kadinda na Wema Sepetu |
Martin
Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema
Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali
yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa,
Kadina alisema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo
kishkaji zaidi.
Akizungumza na Visa Martin alisema ......
"Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachofanya nahangaika kutafuta
deals ili mimi na yeye, maisha ni tusilale njaa, maisha ni kutegemeana"
Martin
aliongeza kwa kusema "kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi
nyingi ili tuwezu kupeana pasu kwa pasu lakini si mshahara, nafanya kazi
na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu"
Martin
alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi
asingemudu na kusema yupo na Wema kwasababu anajua ni mtu wa aina gani
na anafanya akzi zake kwa uhuru bila kubanwa.
Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo wa Ikulu aliyejulikana kwa
jina la Clement(CK) Wema alidaiwa kumwaga pesa kila kona na wapambe
kibao wa kula bata nao hukua akiwa na magari kadhaa lakini kwasasa
anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe
aliokuwa nao wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani.
Hivi karibuni tena Diamond Platnumz aliye mpenzi wa Wema alisema kuwa
Wema ni mtu wa starehe na kuendekeza mashoga wapenda anasa badala ya
kutumia fursa na umaarufu mkubwa alionao sasa kufanya kazi zake kwa
bidii hususani filamu.
Martin Kadinda; Wema Sepetu Hana Pesa Ya Kunilipa, Nahangaika Ili Tusilale Njaa
Reviewed by CapchaMuzic
on
13:52:00
Rating: