Johari adai hajawai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray
Msanii mkongwe wa filamu nchini, Blandina Chagula maarufu kama
Johari, ambaye ni ‘business partner’ wa msanii mwenzake, Vicent Kigosi
aka Ray, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na Ray pamoja na
mipango yake ya kuolewa.
Akizungumza na Bongo5 leo, Johari amesema anashangazwa kuwaona watu wakivumisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ray.
“Mimi
na Ray cha kwanza ni mtu na swahiba wake, cha pili ni kama kaka yangu
kwasababu tumekaa kwa muda mrefu sana. Tumefanya kazi kama partner
wangu, tuna ukaribu ambao upo kikazi zaidi na kampuni yetu, lakini
uhusiano mwingine ambao watu wanauzungumzia sidhani kama upo ni maneno
ya watu,” amesema. “Hatujawahi kutokea uhusiano wa kimapenzi na Ray.
Unajua kuna watu wanaongea vitu vya kubuni, mimi na Ray tunafanya kazi
kampuni moja na wote ni wakurugenzi kwahiyo ina maana tungekuwa tuna
ugomvi tungevunja kampuni. Lakini kitu kama hicho hakipo na bado
tunafanya kazi vizuri na tunaheshimiana na kila mmoja kampuni inampatia
maisha mazuri. Kwa sasa sijaolewa lakini siwezi kuweka wazi sana
mahusiano yangu kwa sababu muda haujafika ila muda utakapofika
tutawaweka watu wazi. Nitawaweka wazi hivi mbioni kwa sababu zangu.
Inaweza ikawa ni mapema zaidi ila natawataka watu wasubiri ili waone
nini kitatokea,” aliongeza Johari.
Pia Johari alizungumzia jinsi ambavyo wanashare kampuni ya RJ pamoja na mipangilio ya kutoa kazi zao.
“Kazi
zangu zote ninazotoa zinatoka ndani ya RJ Company lakini kwa sababu
kwenye kampuni ni yetu wote na wote ni wakubwa tunapishana katika kutoa
kazi,” anasema. “Pia hata wasanii ambao wanafanya kazi kwenye kampuni
yetu tunajaribu kupishanisha ili kuleta manufaa mazuri katika kazi
tunazofanya. Kampuni ya RJ Company ni kampuni mbayo imesajiriwa ina TIN
namba, yaani ni kampuni kama kampuni nyinge kubwa na sidhani kama
inaweza kuvunjika kwa sababu tulikotoka na tulipo sasa hivi ni mbali
sana. Kwahiyo kampuni kama kampuni inafanya kazi zake vizuri na haiwezi
kuvunjika leo wala kesho kwakuwa kila mtu ananufaika vizuri na hiyo
kampuni.”
Johari adai hajawai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:26:00
Rating: