Hii ndo namba ya Freemason nayoitumia Ney wa Mitego mpka kuichukulia Gari
Kama wewe ni msikilizaji wa nyimbo za mkali wa bongofleva Nay wa Mitego nina uhakika utakua umeisikia sana namba 966 ambayo huitaja sana kwenye mashairi yake lakini mpaka sasa hajawahi kusema ina maana gani.
Kwenye exclusive na millardayo.com
juzi Nay alisema kuna siku tu atakuja kueleza maana ya hii namba pamoja
na baadhi ya alama ambazo amekua akizitumia kwenye picha zake za video
ambazo zimesababisha Mama yake mzazi kumuita na kutaka amweleze zina
maana gani manake amekua akisikia watu wengi wakimuusisha Mwanae na imani ya Freemason
Pamoja
na kwamba wengi walianza kuzihusisha hizi alama na hii namba imani ya
kuabudu Miungu, Nay amesema hayuko kwenye dhehebu lolote ambalo
linaabudu Miungu, watu wavute subira iko siku atasema kila kitu ikiwemo
mipango yake na hii namba ambayo inaonekana ameiandalia kitu kikubwa
mpaka kulichukulia gari lake jipya.
Hii namba unayoiona hapa kwenye picha ya kwanza haijamuangukia bahati
mbaya bali alifanya namna mpaka akaipata wakati wa kwenda kusajili gari
lake kwenye mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
Hii ndo namba ya Freemason nayoitumia Ney wa Mitego mpka kuichukulia Gari
Reviewed by CapchaMuzic
on
06:09:00
Rating: