CRDB YAIPA YANGA MIAKA MITANO TU KUWA TAJIRI KAMA MANCHESTER UNITED
BENKI
ya CRDB imesema ndani ya miaka mitano Yanga SC inaweza kuikaribia
kiuchumi Manchester United ya England, iwapo wanachama wake watatumia
vizuri fursa ya kuichangia klabu yao kupitia benki hiyo.
Yanga
SC imeingia Mkataba huru wa kuanzia na benki ya CRDB kwa ajili ya
kuchapisha kadi mpya za wanachama wake, zitakazojulikana kama Gold Card
baada ya kuachana na beki ya Posta.
Mkurugenzi
Mtendaji wa DRCB, Dk Charles Kimei ametiliana saini Mkataba huo na
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Mama Fatuma Karume leo
katika ofisi za benki hiyo, Mtaa wa Azikiwe, Dar es Salaam.
Kimei
amesema kwamba kadi hizo zitapatikana kwa gharama ya Sh. 8,000 lakini
kwa wateja wapya ambao ni wanachama wa Yanga SC watapatiwa bure.
Amesema
malengo waliyojiwekea CRDB ni kukusanya wanachama 100,000 ndani ya mezi
ya miwili kwa kuanzia. Amesema wanachama wa Yanga SC wanaweza
kuichangia klabu hiyo kiasi chochote cha fedha kwa matakwa yao kulingana
na uwezo wao.
“Endapo wanachama wa Yanga watachangamkia kadi hizi na kulipa michango yao, Yanga inaweza kuwa na nguvu ya kiuchumi kiasi hata cha kuikaribia Manchester United ndani ya miaka mitano tu,”amesema Kimei. Amesema anaamini Yanga SC ni klabu kubwa na ina wanachama wengi na kwamba hata baadhi ya wateja wake ni wanachama wa klabu hiyo. Amesema huduma hiyo inapatikana nchi nzima katika matawi yote ya benki ya CRDB. Kwa upande wake, Mama Karume, mke wa rais wa zamani wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume (sasa marehemu) ameishukuru CRDB kwa kuisaidia Yanga SC katika hilo na akawapongeza viongozi kwa juhudi zao za kuipata benki hiyo. Juni mwaka huu, Yanga SC iliingia Mkataba wa aina hiyo na benki ya Posta, lakini imeamua kuachana nayo kwa madai malengo hayajatimia.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Lukumai kulia akiwekeana saini ya Mkataba na Mama Fatuma Karume. |
“Endapo wanachama wa Yanga watachangamkia kadi hizi na kulipa michango yao, Yanga inaweza kuwa na nguvu ya kiuchumi kiasi hata cha kuikaribia Manchester United ndani ya miaka mitano tu,”amesema Kimei. Amesema anaamini Yanga SC ni klabu kubwa na ina wanachama wengi na kwamba hata baadhi ya wateja wake ni wanachama wa klabu hiyo. Amesema huduma hiyo inapatikana nchi nzima katika matawi yote ya benki ya CRDB. Kwa upande wake, Mama Karume, mke wa rais wa zamani wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume (sasa marehemu) ameishukuru CRDB kwa kuisaidia Yanga SC katika hilo na akawapongeza viongozi kwa juhudi zao za kuipata benki hiyo. Juni mwaka huu, Yanga SC iliingia Mkataba wa aina hiyo na benki ya Posta, lakini imeamua kuachana nayo kwa madai malengo hayajatimia.
CRDB YAIPA YANGA MIAKA MITANO TU KUWA TAJIRI KAMA MANCHESTER UNITED
Reviewed by CapchaMuzic
on
03:34:00
Rating: