Video: Mizengo Pinda apewa shavu kwenye The Colbert Report ya Comedy Central.. lakini si kama unavyodhani
Kutajwa kwenye show kubwa inayotazamwa kwenye channel ya TV
inayoangaliwa mno nchini Marekani, Comedy Central si kitu cha kuchukulia
poa hasa kama aliyetajwa ni Mtanzania.
Mtangazaji
wa kipindi cha The Colbert Report, Stephen Colbert jana amempa shavu
waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda wakati akikikosoa kitabu cha mke
wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, Hillary Rodham Clinton
‘Hard Choices’.
Colbert anadai kuwa pamoja na kitabu hicho kuwa na
kurasa 656, kimejaa utajaji hovyo wa majina huku sehemu moja akisema
‘Mimi na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda tunapanda miti kwenye
chama cha wanawake huko Mlandizi’.
Hata hivyo mtangazaji huyo
aliwasurprise zaidi watazamaji aliposema: “There is no way on earth one
woman can be in so many places at once’ na muda huo Clinton akaingia
studio hapo na kusababisha shangwe zito.
Video: Mizengo Pinda apewa shavu kwenye The Colbert Report ya Comedy Central.. lakini si kama unavyodhani
Reviewed by Unknown
on
08:00:00
Rating:
Reviewed by Unknown
on
08:00:00
Rating: