Umeisikia BongoIceChallenge ? hii inakuhusu kama wewe ni mtanzania !!!!

Kama wewe ni mjanja basi utakua umeshaisikia  ALS  ice bucket challenge na umeshaona watu maarufu wakijimwagia maji basi usidani huu ni mchezo bali ni aina fulani ya kampeni ambayo inaendelea kufanyika katika kuchangia mfuko wakusaidia watu wenye matatizo ya ugonjwa maarufu ujulikanao kama ALS, ugonjwa huu huenda kuharibu nerve cells ambapo mgonjwa anayepatwa anakuwa anashindwa kutembea na mwisho wa siku anakuwa amepooza kabisa.Mtu akikucgagua kutekeleza kampeni hii unaweza kujimwagia maji au kutoa mchango wa fedha au kufanya vyote ndani ya masaa 24.
BongoIce-Challenge-Vodacom

Vodacom Tanzania na wenyewe wameamua kuanzisha kampeni  yao inayoitwa BongoIceChallenge ambapo utekelezwaji wako upo sawa na IceBucketChallenge sema tofauti yake ni kwamba  kwa hii ya bongo itakua inalenga kuchangia wagojwa wa fistula , ugonjwa ambao ni tatizo kubwa sana hapa nchini. Kwa kutambua hilo mkurugenzi  kurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza ameshiriki BongoIceChallenge huku akiwachagua January Makamba , mkurugenzi mtendaji wa Tigo Tanzania na Airtel Tanzania na wengine kushiriki ndani ya masaa 24 au kuchangia pesa ambapo kwa upande wake amefanya vyote huku akichangia dola 100.
Umeisikia BongoIceChallenge ? hii inakuhusu kama wewe ni mtanzania !!!! Umeisikia BongoIceChallenge ? hii inakuhusu kama wewe ni mtanzania !!!! Reviewed by Unknown on 09:57:00 Rating: 5
Powered by Blogger.