Ukiona mwanamke ana tabia hizi,basi ujue ni kicheche.

Anamarafiki wakiume kwa faida.
Kwa mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo ishu, ila ishu ni pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume, na kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale, ila kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo cheche.
Lifestyle-wanaume

Anakasirika haraka usipompa anachotaka.
Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe week nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.
Lifestyle-demu-anataka
Siyo rahisi kupenda.
Wanawake vicheche huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano, wanataka siku zote wawe available ili kwa mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye, na hata akiamua kupenda, huwa hakai sana, labda kama unamsaidia asilimia 90% ya matatizo yake.
Lifestyle-demu-kicheche
Anachukulia mahusiano kama biashara.
Watu kama hawa huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako.
lifestyle-demu-anataka-zawadi
Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo.
Kwa mwanamke kicheche, pale tu utapomchekea na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka.
lifestyle-demu-anategeka
Ukiona mwanamke ana tabia hizi,basi ujue ni kicheche. Ukiona mwanamke ana tabia hizi,basi ujue ni kicheche. Reviewed by CapchaMuzic on 00:25:00 Rating: 5
Powered by Blogger.